Home Habari za Yanga Leo YANGA YAONGEZA MWINGINE…USAJILI WA DAMU CHANGA

YANGA YAONGEZA MWINGINE…USAJILI WA DAMU CHANGA

HABARI ZA YANGA LEO.

KATIKA msafara wa Yanga ulioondoka juzi kuelekea Afrika Kusini kuna bosi mpya wamemjumuisha aliyeanza kazi kimyakimya.

Kwenye msafara huo wa Yanga uliongozwa na Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said ndani kuna mtu mpya Ibrahim Mohammed.

Mohammed ametua Yanga akitarajiwa kutambulishwa kama Mkurugenzi mpya wa Idara ya Mashindano ya timu hiyo, klabu hiyo ikivutiwa na uzoefu wake.

Ingawa Yanga bado hawajatoa taarifa rasmi lakini tayari Mohammed yuko na timu hiyo nchini Afrika Kusini na kikosi cha timu hiyo.

Mohammed anatua Yanga akitokea Kagera Sugar alipokuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, ambapo aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika mara baada ya msimu wa Ligi Kuu uliopita kumalizika.

Kigogo huyo pia amewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiwa kwenye idara ya mashindano kabla ya kutimkia Kagera Sugar.

Mohammed anakuwa kigogo wa pili kuchukuliwa na Yanga ambapo mapema mabingwa hao walimchukua Walter Harrison aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa KMC na kwenda kuwa meneja wa timu hiyo.

Klabu ya Yanga imeendelea kujiimarisha zaidi katika eneo la Uongozi, ikiongeza nguvu kwa watendaji wapya na vijana ili kuendana na Mpira wa kisasa.

Benchi la Ufundi la Yanga limekamilika likionngozwa na Miguel Gamondi,  huku pia upande wa wachezaji wa klabu hiyo wakiwa imara kuuanza msimu mpya.

SOMA NA HII  KUHUSU PITSO NA IBENGE KUHUSISHWA NA YANGA ...UKWELI WA MAMBO HUU HAPA...LOLOTE LINAWEZEKANA...