habari za yanga-sasii
Habari za michezo

PILATO WA SIMBA NA YANGA NI ELLY SASII

Abubakar August 6, 2024 5:41 pm

Mwamuzi Elly Sasii amechaguliwa kuchezesha mechi ya Kariakoo Derby kati ya Young Africans dhidi ya Simba mnamo Agosti 8, 2024 katika dimba la Mkapa.

Mwamuzi Ahmed Arajiga atachezesha mechi ya Azam dhidi ya Coastal Union mnamo Agosti 8, 2024.

WAAMUZI NGAO YA JAMII
AGOSTI 8, 2024

AHMED ARAJIGA:
Azam FC vs Coastal Union
Saa 10.00 Jioni
Aman Stadium

ELLY SASII:
Yanga SC vs Simba SC
Benjamin Mkapa
Saa 1.00 usiku.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa Simba na Yanga kukutana kwa msimu huu wa 2024/25.

Na huenda kwa msimu huu  timu hizo zikakutana zaidi ya mara tatu,  ambapo msimu ulioisha 2023/24 Simba na Yanga, walikutana mara 3, ambapo Yanga ilishinda mara 2 na Simba ilifanikiwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti na kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii.

BODI YA LIGI YATOA TAMKO…AHMED ALLY NA WENZAKE KUACHA UCOMEDY JOSHUA MUTALE AWAITA MASHABIKI TAREHE 8…AAHIDI KUWAPA FURAHA