Uchambuzi wa Hans Rafael wa Crown Media kuhusu mchezaji mpya wa Simba, kiungo wa kazi Debora Fernandes Mavambo ambapo, Rafael alimchambua mchezaji huyo kwa kuandika hivi.
Mavambo amebarikiwa umbo kubwa,unyumbulifu na uwezo wa kupiga pasi.
Muda mwingi BMavambo hapendi kuupaka mpira rangi badala yake anapokea mali na kuachia (one touch football) ni ngumu sana kumfanyia pressing mchezaji wa namna hii…ingawa bado hana fitness ya kucheza dakika 90.
Nimefanikiwa kumtazama mechi mbili akiwa na Simba ila nadhani hii bidhaa ya moto kuelekea msimu ujao.