Home Habari za Simba Leo FERNANDES MAVAMBO APEWA MZIGO MKUBWA SIMBA

FERNANDES MAVAMBO APEWA MZIGO MKUBWA SIMBA

Habari za Simba- Mavamo

Debora Fernandes Mavambo unaweza kusema amekabidhiwa mikoba mizito  kutokana na uzi atakaotumia kuwa na namba iliyoacha rekodi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Debora Fernandes Mavambo kwa sasa pale Simba anavaa jezi namba 17, ambayo ilikuwa inavaliwa na Mwamba wa Lusaka Clatous Chama.

Kwa sasa Chama ameondoka Simba na kujiunga na watani zao Yanga,  lakini akiwa  huko Yanga ameendelea pia kuivaa jezi namba 17.

Tangu awe Simba Chama alifanya mambo makubwa sana akiwa na jezi hiyo  mgongoni mwake,  kwa misimu mitano aliisaidia timu hiyo kutwaa mataji mengi

Ikiwemo Ubingwa wa Ligi Kuu mara 4, ubingwa wa FA mara 2, na Ubingwa wa Mapinduzi mara 2, Ngao ya Jamii mara 2, Kuifikisha Simba hatua ya robo fainali Klabu  Bingwa mara 4 na Kombe la Shirikisho mara 1.

Mavambo Fernandes licha ya presha kubwa ju ya jezi hiyo,  lakini alijitambulisha vyema kabisa katika mechi ya kwanza ya Simba Day,akifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Mavambo Fernandes alipiga shuti  kali nje ya 18 na kufunga, huku aina yake ya uchezaji ukiwavutia wapenzi na mashabiki wa Mnyama.

Ni mchezaji ambaye anamuda kucheza namba Zaidi ya 1, anacheza kama kiungo wa chini, kiungo mshambuliaji na kiungo mchezeshaji.

Swali ni Kwamba ataweza kuitendea haki jezi namba 17? Muda utaongea Zaidi.

SOMA NA HII  WAKATI IBENGE AIKINUKIA SIMBA....MASTAA HAWA 9 KUPIGWA PANGA MSIMU UKIISHA...