Home Habari za Yanga Leo MZIZE ASAINI MIWILI YANGA…KAMWE AFICHUA

MZIZE ASAINI MIWILI YANGA…KAMWE AFICHUA

Habari za Michezo leo

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe amesema Klabu hiyo imemuongezea mkataba mchezaji wao, Clement Mzize wa kuendelea kusalia klabuni hapo kwa miaka mingine miwili baada ya mkataba wake wa awali kubakisha miezi 6 tu kutamatika.

Mzize amekuwa akiimbwa kwenye vyombo vya habari tangu mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutakiwa na vilabu vya Wydad Casablanca ya Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

“Clement Mzize amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Yanga. Mkataba wake wa awali unaisha June 2025.

“Kwa hiyo ukiacha klabu zote zinazomtaka basi amechagua Yanga SC. Na Yanga SC pia imeachana na wachezaji wote Duniani mpaka inampa mkataba Mzize basi ujue ndio imemchagua na ndio anahitajika Yanga.

“Kama ndoto zenu mnataka Mzize aondoke Yanga basi jambo hilo haliwezekani kutokea kwa sasa. Clement Mzize amechagua kucheza Klabu bingwa Afrika badala ya Kombe la Shirikisho.

“Wachambuzi wengi walikua hawampi nafasi Mzize ndani ya Yanga na wakampa maangalizo mengi sana lakini Yanga tukamvumilia kijana, lakini sasa waliokua wanamkataa Mzize ndio wanaoshinikiza kijana aondoke.

“Nitafutieni timu kubwa Afrika kama Al-Ahly, Mamelodi na zingine Duniani kama Real Madrid ambayo inawaachia wachezaji wake muhimu kwenye kikosi, basi sisi ndio kama hao. Sisi ni wakubwa Africa na tunataka kufanya vizuri Africa.

“Kwasasa mnaishi ndoto mlio kuwa hamuioni ikitokea, yaani Wydad Casablanca na wao watakuwa wanakesha kumtafuta mchezaji wa Young Africans na Yanga inakuwa haitaki biashara na mchezaji anawaambia nipo hapa nafurahia maisha, hili jambo hamkuwa mkiliona likija kutokea.

“Pesa sio kila kitu kwa sasahivi kwa Yanga SC, tunachokitafuta ni kutimiza sio ndoto tu za Yanga SC bali ndoto ya taifa hili ya kuona Kombe la afrika linakuja nyumbani ndio tunachokitafuta, sio Wydad Casablanca tu na sio Clement Mzize tu ofa zimekuja nyingi kutoka klabu nyingi,” amesema Ali Kamwe.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIMNGOJA KWA HAMU MANZOKI....BUMBULI ATUPIWA VIRAGO KIMYA KIMYA...MRITHI WAKE NI HUYU HAPA....