Home Habari za Simba Leo FEI TOTO AGOMEA MKATABA MPYA…ANAITAKA SIMBA

FEI TOTO AGOMEA MKATABA MPYA…ANAITAKA SIMBA

HAABRI ZA YANGA- FEISAL

KLABU ya Azam FC jana ilikuwa uwanjani kucheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu kwa msimu wa 2024-2025 dhidi ya JKT Tanzania, lakini kabla ya mechi hiyo, mabosi wa timu hiyo wameshtushwa na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuzuia kwa muda mazungumzo ya mkataba mpya.

Fei Toto alisaini mkatamba wa miaka mitatu ndani ya kikosi hicho, hivyo amebakiza mkataba wa takriban mwaka na miezi kadhaa, jambo ambalo liliwafanya matajiri wa klabu hiyo wajihami mapema kwa kutaka kumuongezea mkataba mpya, lakini walichokutana nacho kimewashitua baada ya kiungo huyo kuwagomea.

Inshu Iko hivi…Mabosi hao walitaka Fei Toto apewe mkataba mrefu zaidi kutokana na kiwango alichokionyesha msimu uliopita na mechi za msimu huu, lakini mchezaji huyo amewataka wasiwe na haraka naye kwa sasa.

Azam ilitaka kumpa mkataba mnono Fei Toto ambao ungemfanya kuwa kiungo ghali zaidi katika Ligi Kuu, hasa baada ya kuifungia timu hiyo mabao 19 akimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Stephane Aziz Ki.

Fei Toto kwa nyakati tofauti amekuwa akihusishwa zaidi na wapinzani wa Yanga na Azam FC, klabu ya Simba ambao walienda na kuuliza uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo katika dirisha kubwa la usajili lililofungwa.

Lakini gharama za mkataba wake zilikuwua ni kubwa mno, hali iliyowarudisha nyuma Simba kwenye mpango wao wa kuinasa saini ya mchezaji huyo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO...SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI...ZAGOMBANIWA KWA NJUGU....