Home Meridianbet NI ZAMU YA MBEZI JUU LEO …..

NI ZAMU YA MBEZI JUU LEO …..

Meridianbet

Mwenge hauvuki kijiji ndio kauli nzuri unayoweza kuitumia kama wengine walifika Mbezi wao ni kina nani wasifikiwe leo imekua zamu yao kufikiwa na mabingwa wa kubashiri kampuni ya Meridianbet.

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri leo wamefika katika eneo la Mbezi na kutoa msaada wa vifaa vya michezo, Ambapo wamefanikiwa kutoa mipira ya kuchezea kuhakikisha wanasaidia vijana kuendelea kuonesha vipaji vyao bila tatizo lolote.

Kama ambavyo inatambulika serikali inajitahidi kuhakikisha inainua sekta ya michezo kwakua ni moja ya sekta ambazo zimekua zikitoa ajira kwa vijana, Hivo Meridianbet wameamua kuinga mkono serikali kwa kuhakikisha nao watoa ushirikiano katika kukuza michezo nchini na ndio sababu wametoa msaada wa mipira leo katika eneo la Mbezi.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Ingram alikua mbele kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na kusema “ Nina furaha kubwa kuwepo mahali hapa leo na kama mnavyojua michezo imekua moja ya sekta muhimu kwa vijana kupata ajira siku hizi, Hivo sisi tumeamua kuhakikisha tunawashika mkono vijana wa eneo hili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika suala zima la michezo haswa mpira wa miguu”

Aidha Diwani wa Jimbo la Mbezi ya Juu Mheshimiwa Anna Lukindo alikuwepo katika zoezi hilo bila kusita alizungumza machache “ Kiukweli niwashukuru sana Meridianbet kwa kufika hapa leo na kuweza kutoa msaada wa vifaa vya michezo ambavyo vitawasaidia vijana wetu wanaopenda michezo kufikia malengo yao, Lakini pia nipende kutoa rai kwa makampuni mengine wanaweza kuiga haya mazuri ambayo yanafanywa na Meridianbet kuhakikisha wanaisaidia jamii yao”

SOMA NA HII  MTOTO HATUMWI DUKANI...FAINALI YA UEFA REAL MADRID vs BORUSSIA DORTMUND