Habari za Simba Leo
FADLU, AHOUA WATAMBA TUZO ZA MWEZI AGOSTI
admin
September 2, 2024
6:09 pm
Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids ameibuka kuwa Kocha bora kwa Mwezi August ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Fadlu aliwashinda Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdallah Mohamed wa Mashujaa alioingia nao fainali katika mchakato huo.
Aliiongoza Simba SC kushinda michezo miwili na kujikusanyia alama sita, ikiwa na jumla ya mabao saba ya kufunga na haijaruhusu bao, hivyo kukaa killeni mwa msimamo wa ligi.
Lakini pia kiungo wa Simba Jean Charles Ahoua ameibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti, hii inakuwa tuzo ya pili kwa mchezaji huyo ya kwanza alichukua kama mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Fountain Gates FC, ambapo Simba ilishinda bao 4-0.
Ahoua katika mchezo huo alihusika kwenye mabao yote 4, akifunga bao moja na kutoa pasi za magoli 2, hukua akianzisha shambulizi la goli jingine pia.