“Nimemsikiliza vyema mwanasheria wa Fountain Gate. Kimsingi nimependa sana jamaa amechagua kuwa mwaminifu.”
“Kimsingi amethibitisha kuwa mkataba baina ya Yanga na Fountain Gate upo tofauti na wengi wanavyosema hakukuwa na mkataba”
“Sasa mwanasheria anapaswa atujibu kwa mujibu wa kanuni na sio maneno, ili mkataba uhesabike umevunjika kutokana na sababu za malipo kanuni za fifa zinasemaje?
Pengine hajui na kwa faida ya wengi acha tumsaidie hapa
“Kanuni ya 12 (1) inaweka jukumu kwa vilabu kutumizia majukumu yao ya kifedha ya kimkataba. Na Yanga tumetimiza hilo na barua yao inathibitisha walipokea malipo ya 30m.”
Je ukichelewa kulipa kanuni inasemaje?
“Kanuni ndogo ya pili inasema klabu yoyote itakayochelewesha malipo kwa zaidi ya siku 30 kwa mchezaji au kwa klabu nyingine basi itakuwa imefanya kosa na itawekewa vikwazo. Zingatia neno VIKWAZO.”
“Kanuni ndogo ya tatu ikaongeza kuwa mhusika atahesabika ana deni. Hakuna mahali imesema mkataba ni batili. Kimsingi huo Mkataba utaendelea kutambulika.”
“Kanuni hiyo ikaendelea kwa kusema, klabu inayodaiwa itapewa siku 10 kwa maandishi kuhusu kulipa deni hilo. Yaan hakuna mahali kanuni inasema eti wakichelewa kulipa basi muuzeni kwingine. NO. Inasema tuma notisi na ukitoa angalau siku 10 za kulipa hela hiyo.”
“Kanuni ikaenda mbali zaidi na kutoka adhabu ambazo zinapaswa kutumika endapo mdaiwa atashindwa kulipa kwa wakati, kwanza kutoa onyo kali, kufungiwa usajili. Lakini hakuna mahali inasema mkataba huo unakuwa umevunjika.”
“Sasa turudi kwa Singida/Fountain Gates FC. Je Yanga walichelewa kulipa kwa muda wa siku 30? Je Singida wakituma notisi ya siku 10? Je kanuni ya kuvunja mkataba kwa kucheleweshwa malipo inasema mkataba huo uvunjike? Au Mwanasheria hasomi kanuni za FIFA? Au hazijui?”