Home Habari za Simba Leo MAREFA WA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA NI HAWA

MAREFA WA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA NI HAWA

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

Marefa kutoka Guinea na Mauritania ndio wamepangwa kuchezesha mechi za nyumbani za wawakilishi wa Tanzania, Simba na Yanga katika mechi zao za marudiano za raundi ya pili ya mashindano ya klabu Afrika.

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba dhidi ya Al Ahly Tripoli utachezeshwa na refa Abdoulaye Manet kutoka Guinea mwenye umri wa miaka 34.

Manet atasaidiwa na Waguinea wenzake ambao ni Sidiki Sidibe, Yamoussa Sylla na Bangaly Konate.

Huo ni mchezo wa kwanza wa mashindano ya klabu Afrika kwa Manet kuchezesha ambapo kabla ya hapo kitu pekee cha kujivunia kwa refa huyo kilikuwa ni kuwa refa wa akiba.

Katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya timu hizo kutoka sare tasa katika mchezo wakwanza uliofanyika Libya, Jumapili iliyopita.

Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00, Jumapili.

Refa wa kati kutoka Mauritania, Abdel Aziz Bouh yeye ameteuliwa na Caf kuchezesha mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na CBE ya Ethiopia.

Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar siku ya Jumamosi, Septemba 22 kuanzia saa 2:30 usiku.

SOMA NA HII  YANGA YAPEWA SIKU 45 NA FIFA...YATAKIWA KULIPA DENI...ITAFUNGIWA USAJILI MISIMU MITATU