Habari za Yanga leo
Habari za Simba Leo

MWAMNYETO AKUBALI KUHITAJIKA SIMBA

Abubakar September 18, 2024 12:11 pm

NAHODHA wa Yanga SC Bakari Mwamnyeto amethibitisha kuwa ni kweli klabu ya Simba SC ilimuhitaji kumsajili kwaajili ya kujiunga na kikosi chao katika msimu huu mashindano wa 2024- 2025.

“Viongozi wa Simba SC walikuwa wanaongea na Meneja wangu kwa muda wote lakini mimi ni mchezaji natafuta maisha kwahiyo sehemu yoyote mambo yakienda vizuri nacheza” amesema Bakari Mwanyeto Nahodha wa Yanga SC.

Katika dirisha kubwa baada ya Simba kumsajili Lameck Lawi walikuwa wanapushi sana kuipata saini ya Mwamnyeto, lakini mambo yakaenda kombo akaongezwa mkataba na Yanga huku akipewa mshahara mnono wa Mil 10.

Simba ili kutafuta mbadala wa Mwamnyeto waliamua kuingia sokoni haraka, ndipo walipompata kijana hatari Abdulrazak Hamza ambaye amekuwa na kiwango bora sana kwenye mechi alizopewa nafasi ya kucheza.

DUBE AANZA KUSUKWA UPYA…APEWA MBINU HIZI NA GAMONDI MAREFA WA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA NI HAWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “MWAMNYETO AKUBALI KUHITAJIKA SIMBA”

  1. […] wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto amesema kuwa makosa ambayo yalitokea kwenye mchezo uliopita ugenini licha ya kupata ushindi […]