Home Habari za Simba Leo RALLY BWALYA AWAPA SIRI SIMBA…KUIMALIZA AL AHLI

RALLY BWALYA AWAPA SIRI SIMBA…KUIMALIZA AL AHLI

HABARI ZA SIMBA-BWALYA

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids anaamini wachezaji wake wanaweza kufanya vyema katika mchezo huo wa maamuzi dhidi ya Al Ahli Tripoli.

“Itakuwa mechi tofauti kabisa, tutatakiwa kuwa na nidhamu kubwa katika kulinda na kushambulia. Tuna faida ya kuwa nyumbani, hivyo nitoe wito kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi. Itakuwa mechi nzuri na kuvutia, kwetu ni kama kazi itaanza upya.”

RALLY BWALYA AKAZIA

Mchezaji wa zamani wa Simba, Rally Bwalya, hakusita kutoa neno la faraja kwa klabu yake ya zamani. “Nakumbuka jinsi mashabiki walivyokuwa wakitufanya kujituma zaidi kutokana na sapoti yao. Simba ina nafasi ya kwenda makundi,” alisema Bwalya.

Katika mchezo huo wa maamuzi dhidi ya Al Ahli Tripoli, Simba wanajua wazi ushindi utawahakikishia tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Hivyo kocha Fadlu na vijana wake watalazimika kuonyesha nidhamu, umoja na uwezo mzuri wa kiufundi ili kupata matokeo mazuri.

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA...NAHODHA YANGA AFUNGUKA SIRI HII YA KUWACHAPA RIVERS

1 COMMENT

  1. […] BAADA ya ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara mbele ya KMC, Septemba 19 2024 uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa hizo ni salamu kwa mpinzani wao ajaye ambaye ni Simba. […]

Comments are closed.