Home Habari za Simba Leo MALIJENDI WAMPA MINU MUTALE…BWALYA NA DAANY MRWANDA WAHUSIKA

MALIJENDI WAMPA MINU MUTALE…BWALYA NA DAANY MRWANDA WAHUSIKA

HABARI ZA SIMBA- MUTALE

Straika wa zamani wa Simba SC, Athuman Machupa amesema ili Joshua Mutale ajijengee ufalme ndani ya klabu hiyo, kiwango chake kiwe na mchango mkubwa akimsisitiza kwamba azingatie nidhamu na kujituma.

“Soka haliongopi linachezwa sehemu za wazi ambapo kila mtu anaona anachokifanya. Kama Chama alitikisa na jina lake la Mwamba wa Lusaka, Phiri la jenerari, naamini kwa umri wake (Mutale) kama atazingatia nidhamu na kujituma ataishi kwenye ndoto ya jina lake kuwa kubwa,” alisema.

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo, Frank Kasanga ‘Bwalya’ alisema: “Bado hatujaona wachezaji wapya wanavyocheza, ila kwa mechi ambazo nimewahi kumuona ni mchezaji mzuri. Jambo la msingi ajitambue, katika soka nidhamu ndio kila kitu. Akifanya hivyo atafanya makubwa na Wanasimba watamwita Mwamba wa Zambia.”

Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Danny Mrwanda alisema: “Heshima yake Mutale ni rahisi kujengeka endapo tu atafanya majukumu yake ipasavyo, kwani soka halina njia za mkato.”

Mrwanda alisema mchezaji huyo akifanya kazi nzuri mashabiki wanaweza wakampa jina lingine zaidi ya hil la Mwamba wa Zambia, akisisitiza kiwango chake kitampa heshima anayotaka.

SOMA NA HII  MNAWASIFIA SANA MAMELODI SUNDOWNS...WATAPIGWA NA SIMBA MSHANGAE