Home Habari za Yanga Leo DUKE ABUYA APATA MZUKA NA BAO LAKE LA CAF

DUKE ABUYA APATA MZUKA NA BAO LAKE LA CAF

habari za yannga-GAMONDI

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mkenya Duke Abuya juzi usiku alitokea benchi kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar kisha kufunga bao moja kati ya sita yaliyoizamisha CBE SA ya Ethiopia na kumpa mzuka mwingi nyota huyo aliyesema anaona safari ya mabao ndo imeanza sasa kimataifa.

Abuya aliyetokla kufunga bao wakati timu ya taifav ya Kenya, Harambee Stars ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Namibia katika mechi za kufuzu fainali za Afcon 2025, juzi aliingia kumpokea Maxi Nzengeli kipindi cha pili na kufunga bao la tano akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Stephane Aziz KI.

Akizungumza na Mwanaspoti, Abuya alisema alikuwa anatamani kufunga akaunti ya mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Yanga, hivyo kufunga katika mchezo huo, kwake anaona imempa morali zaidi ya kupambana kwa ajili ya huduma yake iwe na manufaa kwa timu.

“Nilikuwa nasubiria kufunga kwa hamu, nimefurahia kuona hilo limetimia, nijiona ndio nimeanza safari ya mapambano, kwani natamani kufunga sana,njia imefunguka, kilichobakia ni kujituma kwa bidii, kwani nafasi ninayocheza ina ushindani mkali,” alisema Duke aliyewahi kukipiga Singida Fountain Gate na Ihefu (sasa Singida Black Stars).

“Mashabiki, viongozi, benchi la ufundi nashukuru kwa sapoti yao, hao ni sababu ya sisi kujituma kwa bidii, ili kufanya kile wanachokitarajia kutoka kwetu,” aliongeza Abuya aliyekipiga pia Mathare United, Kariobang Sharkd na Polisi Kenya, huku akipita pia Nkana FC ya Zambia.

Yanga ilimsajili Abuya kutoka Singida BS, ambapo kwa msimu uliopita alifunga mabao manne, asisti mbili, alicheza dakika 2363, alipiga mipira iliyolenga holini 15 na iliyotoka nje 15.

SOMA NA HII  ISHU YA MAXI KUTAKIWA SIMBA UKWELI HUU HAPA...TIMU YAKE YA CONGO WAANIKA KILA KITU...