Home Habari za Yanga Leo GAMONDI ACHUKIZWA NA KUKOSA MABAO

GAMONDI ACHUKIZWA NA KUKOSA MABAO

habari za yanga-Gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amechukizwa na namna ambavyo wachezaji wake wanavyokosa magoli, licha ya timu yake kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Katika mchezo wa Kimataifa uliopita wikiendi hii, Yanga ilikuwa Ethiopia kucheza dhidi ya Commercial Bank of Ethiopia CBE,  na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1.

Bao hilo lilifungwa na Prince Dube licha ya kukosa sana nafasi nyingi, lakini aliweza kurekebisha makosa yake, na hali hiyo imemfanya Gamondi kuongea kwa uchungu.

“Unawezaje kunyamaza kwa mazingira kama yale, unapotengeneza nafasi unatakiwa kuzitumia kwa wingi, nawaheshimu wapinzani wetu lakini ile ni mechi ambayo tulitakiwa kushinda kuanzia mabao matano,”

“Sio kila wakati utapata nafasi kama zile kisha uje utumie moja, zipo mechi ambazo unaweza kupata nafasi moja au mbili ili uamue mechi, nimewaambia nataka kuona kila mmoja anatuliza akili anapofika eneo ambalo tunatakiwa kufunga.” Allisema Gamondi.

SOMA NA HII  JAMBO JIPYA LA YANGA HILI HAPA...SIMBA HAWAJAWAHI KUFIKIA REKODI HII KAMWE...