Home Habari za Yanga Leo HATIMAYE MTASINGWA AJIBU KUHUSISHWAA NA YANGA

HATIMAYE MTASINGWA AJIBU KUHUSISHWAA NA YANGA

HABARI ZA YANGA-MTASINGWA

KIUNGO wa Azam FC Adolf Mtasingwa, amejibu ule uvumi wa taarifa za yeye kujiunga na Yanga katika dirisha kubwa la usajili.

“MUDA ndio muamuzi wa kila jambo. Mengi yalizungumzwa juu yangu wakati wa dirisha la usajili, lakini wakati umeamua mimi kuwa hapa nilipo,”

Mtasingwa ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Azam FC amethibitisha kuwa ni kweli alikuwa na ofa kutoka Yanga lakini amefanya uamuzi sahihi kubaki Chamazi kutokana na klabu hiyo kumuamini na kuhusu Jangwani, “labda wakati mwingine”. Adolf Mtasingwa.

Katika dirisha kubwa usajili kulisambaa taarifa za kiungo huyo  kuhitajika na Yanga,  ambapo ilielezwa kuwa mchezaji huyo alishasaini mkataba wa awali na Yanga na atajiunga nao dirisha dogo la usajili.

SOMA NA HII  MASTAA WALIOSEPA WAKARUDI BONGO...SIMBA NA YANGA USIPIME