Home Habari za Yanga Leo MBINU 3 ZA KUIZUIA YANGA…SIMBA, AZAM ZAJIPANGA

MBINU 3 ZA KUIZUIA YANGA…SIMBA, AZAM ZAJIPANGA

HABARI ZA YANGA-Injinia Hersi

UMEKUWA ukijiuliza Yanga chini ya Miguel Gamondi wanafanikiwa wapi ndani ya uwanja, hadi kutembeza kichapo cha mabao mengi kwa wapinzani wake, ikumbukwe Yanga kwenye mechi tatu za mashindano, Yanga imefunga jumla ya magoli 12, huku magoli 10 yakifungwa kwenye mechi dhidi ya Vital’o.

Kama unakutana na Yanga leo halafu timu yako ikashindwa kujipanga na mambo matatu makubwa ya ubora wa mabingwa hao watetezi utajikuta unaumia;

UKABAJI

Yanga inaweza kuwa timu inayofanya vizuri kwa mbinu zake uwanjani hasa nidhamu ya wachezaji wake wakati hawana mpira na wakati wanaumiliki mpira.

Yanga inapopoteza mpira haraka inaanzia ukabaji eneo la juu ambapo timu pinzani kwao inapokuwa inamiliki mpira kuna mchezaji mmoja mpaka watatu watapeleka presha ili mpira waupokonye na uwe kwenye umiliki wao.

Endapo timu yako haijajipanga na presha ya namna hii ndio hapo itajikuta kila wakati Yanga inaumiliki mpira na kushambulia kwa nguvu kuelekea langoni kwenu.

KASI YA MASHAMBULIZI

Yanga pia ina kasi kubwa inapokuwa inaishambulia timu pinzani ambapo kama inakutana na timu isiyokuwa na nidhamu nzuri ya kukaba wanaweza kujikuta wanapoteza vibaya.

UBORA WA WACHEZAJI

Mbali na mbinu hizo, Yanga wachezaji wake wana ukomavu mkubwa wa akili katika kuamua matukio ndani ya uwanja, kitu ambacho kimezidhuru timu nyingi.

MWAMBA NI HUYU

Kikosi hicho cha Kocha Miguel Gamondi ubora mkubwa umetoka kwa kocha wao wa mazoezi, Taibi Lagrouni ambaye kazi yake ya kuwaimarisha wachezaji kwa stamina na pumzi ya kutosha ndio inayokwenda kutekeleza kwa urahisi mbinu zao.

Pumzi ya wachezaji wa Yanga ndio inayokwenda kuwapa wepesi kwenye mbinu za Gamondi na kuwapa shida wapinzani wake.

SIMBA WANAJIPANGA

Licha ya falsafa za Kocha wa Simba, Fadlu Davids ambaye kwa mechi ambazo timu yake kuonyesha anataka kuona wachezaji wake wanakaba kwa haraka na kushambulia kwa kasi lakini bado hilo halijafanikiwa.

Simba imeruhusu mabao mawili kutoka mechi ya Yanga ya Ngao ya Jamii lakini pia mchezo wa juzi wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ambapo mabao yote yameonyesha namna wachezaji wa wekundu hao wakionyesha udhaifu wa kukaba kwa nguvu.

Kwenye mchezo dhidi ya Yanga bao ambalo Simba iliruhusu zilipigwa pasi 14 mpaka mpira unaingia nyavuni kupitia kiungo Maxi Nzengeli ikionyesha namna udhaifu wa wachezaji wa wekundu hao kwenye ukabaji.

Wakati Yanga inatengeneza shambulizi hilo kwa pasi za haraka kumbuka Simba ilikuwa na wachezaji tisa kwenye eneo lao lakini ikashindwa kutegua mtego huo mapema na kujikuta inaruhusu bao hilo ambalo ndio lililokwenda kuwaondoa kutetea taji lao la Ngao ya Jamii ililokuwa inalishikilia.

Serge Pokou ambaye aliwafunga Simba juzi wakati akiisawazishia timu yake ya Al Hilal katika mchezo wa kirafiki, Simba walipoteza mpira ndani ya eneo la hatari la wapinzani lakini wachezaji saba wanashindwa kuzuia pasi mbili tu za wachezaji wawili zilizokwenda kutengeneza bao hilo.

SOMA NA HII  MAYELE NA MUSONDA 'WAMCHOMA' NABI....AWAPA ZA USO LIVE KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA...