Home Habari za Simba Leo SEMAJI WA UBAYA UBWELA AANZA FUJO…ATAMBA NA MASHINE ZAO

SEMAJI WA UBAYA UBWELA AANZA FUJO…ATAMBA NA MASHINE ZAO

Habari za Simba

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wote waliopo ndani ya kikosi cha Simba wapo tayari kupambania uzi wa Mnyama na kuwapa furaha Wanasimba.

Msimu wa 2023/24 Simba ilimaliza ligi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya mechi 30 ikiwa na pointi 69 itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Coastal Union ya Tanga iliyogotea nafasi ya nne.

Yanga ambao ni mabingwa wa ligi na Azam FC iliyogotea nafasi ya pili hizi itakuwa kwenye anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya Simba ni Deborah Fernandez, Edwin Balua, Mzamiru Yassin, Mhamed Hussein, Ayoub Lakred, Camara Mousa, Kibu Dennis.

“Wachezaji wote wa Simba wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 na tunatambua kwamba msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu kutokana na kushindwa kufikia malengo yetu lakini tunaanza upya kuyakimbiza malengo yetu hilo inawezekana.’

Agosti 8 2024 ni Kariakoo Dabi, Simba v Yanga katika Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa na Coastal Union itacheza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa New Amaan Complex fainali itachezwa Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  BALEKE AWAPA NAFASI ZAIDI YANGA, SIMBA...NIPO TAYARI KURUDI SIMBA