Home Habari za michezo SIMBA,YANGA, AZAM & COASTAL…ZATAKIWA KUKAMILISHA USAJILI HARAKA

SIMBA,YANGA, AZAM & COASTAL…ZATAKIWA KUKAMILISHA USAJILI HARAKA

Habari za yanga leo

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezitaka timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kukamilisha sajili zao mapema. Timu hizo ni Simba, Yanga, AZAM FC na Coastal Union.

CAF Imeonesha kalenda ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, huku ikionekana kuwa ratiba ya msimu huu imebana, hivyo muda uliopo ni mchache sana kwa usajili.

Tanzania imefanikiwa kupata nafasi ya kuingiza timu nne kwenye mashindano ya Kimataifa, Yanga SC, Azam FC watakipiga Ligi ya Mabingwa, huku Simba SC na Coastal Unioni kukipiga Shirikisho.

Kwa mujibu ya ratiba ya CAF inaonesha mchakato wa kuanzia mwanzo wa mashindano hayo hadi siku ya fainali ya msimu wa 2024/2025, inaonyesha kuwa hatua ya awali mechi zake zitaanza Agosti 16 na 18, huku hatua ya makundi ikitarajiwa kupigwa Oktoba hadi Desemba 2024.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa fainali italazimika kuwa Mei mwaka 2025 mfumo ukiwa uleule wa nyumbani na ugenini.

Hii ina maana kuwa timu za Azam na Coastal Union ambazo zinaonekana kuwa zitaanzia hatua ya awali zinatakiwa kuhakikisha zimekamilisha usajili wake hadi Julai 20, huku zile za Simba na Yanga ambazo zitacheza hatua ya kwanza zikipewa kutoka Julai 21 hadi Agosti 31 kuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha usajili wake Caf.

Hii ina maana kuwa timu za Azam na Coastal zinatakiwa kuanza mchakato wa usajili sasa kama zinataka kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kwa usajili wa Tanzania dirisha lake linatarajiwa kufunguliwa Juni 15 ambalo litakwenda hadi Agosti 31, mwaka huu.

Hata hivyo, shirikisho hilo limeendelea kuweka mkazo kuwa hakuna timu ambayo itatolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikashuka Shirikisho ukiwa ni mfumo kama ambavyo ulikuwa msimu uliopita.

Kwa upande wa usajili katikati ya mashindano umeonekana kuwa timu ambazo zitafanikiwa kuingia hatua ya makundi zitapewa nafasi ya kusajili wachezaji wapya saba huku usajili huo ukifunguliwa Januari Mosi na kufungwa Januari 31, 2025.

“Utaratibu huu wa usajili umefanyika ili kuhakikisha kila timu inapata nafasi ya kushiriki kwa usawa kwenye hatua zote za mashindano haya,” Ilisomeka sehemu ya taarifa ya CAF.

SOMA NA HII  HII HAPA WIKIENDI YA KUCHOTA MIHELA NA MERIDIANBET...KILA MECHI INA ODDS ZA KUSHIBA...