Home Habari za Yanga Leo RAIS WA FIFA AIPONGEZA YANGA…HABARI ZA YANGA DUNIANI KOTE

RAIS WA FIFA AIPONGEZA YANGA…HABARI ZA YANGA DUNIANI KOTE

rais wa fifa- Aipongeza Yanga

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za pongezi kwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 Klabu ya Yanga SC.

Infantino amesema juhudi zao katika msimu mzima zimezaa matunda na kupata taji hilo muhimu huku akiwapongeza wanachama wote wa Klabu hiyo kwa mafanikio hayo.

Aidha amemshukuru Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kazi nzuri na kujitolea kwa maendeleo ya mpira wa miguu wa Tanzania.

Msimu uliomalizika wa 2023/24 klabu ya Yanga SC imeendeleza ubabe wake wa kutetea mataji yake muhimu, Kombe la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho, kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupita miaka takribani 20.

Pia Yanga baada ya kufika hatua ya makund walipangwa kundi gumu, lenye miamba kama Al ahly ambaye ndiye bingwa wa sasa wa Ligi ya Mabingwa, Madeama ya Ghana na CR Belouzdad lakini walifanikiwa kutoboa na kucheza hatua ya robo fainali, ikiwa ni mara yao ya kwanza.

Safari yao kwa msimu wa 2023/24 Kimataifa iliishia hatua ya robo fainali, ambapo Masandawana kutoka Afrika ya Kusini ndiyo waliohusika kukatiza ndoto za wananchi kucheza nusu fainali au hata fainali, kwani kikosi cha kumfikisha huko alikuwa nacho.

Baada ya msimu kuisha na Yanga kunyanyua mataji yote muhimu ya ndani, Rais wa klabu hiyo Eng Hersi alisema, atafanya usajili wa maana kwa msimu huu ili kukiboresha kikosi chake kwa msimu ujao wa mashindani ya ndani na ya Kimataifa.

SOMA NA HII  VITA HII MPYA YAIBUKA YANGA...BACCA AMPASUA KICHWA JOB...ISHU NZIMA IKO HIVI