Home Habari za Yanga Leo MOURINHO ARUDI YANGA…MAISHA YAKE NJE YA SOKA

MOURINHO ARUDI YANGA…MAISHA YAKE NJE YA SOKA

habari za yanga-Mourinho

Siku naongea na Edna Lema Mourinho wa Bongo mara ya kwanza sikujua kama anaweza kwenda Kuishi na kufundisha team ya wanaume tena mkoani Mara.

Alikubali kwenda Musoma kufanya kazi ya kuifundisha Biashara Utd ya Mara kama kocha msaidizi akiwa na elimu ay juu ya coaching CAF Diploma A, na akiwa na uzoefu kwenye mpira wa Tanzania zaidi ya miaka 20.

Uzoefu wake na elimu yake niliamini atakuwa msaada mkubwa kwenye team yetu hivyo nilikuwa na uhakika kuwa atafanya kazi nzuri kwa kushirikiana na wenzake.

Nilichojifunza Huyu mama hakuwa Kocha tu bali alikuwa mama mlezi na aliamua kujitoa kwa moyo wake wote akawa zaidi ya kocha, nilijikuta namchukulia kama mshauri wangu kwenye masuala ya uendeshaji wa Timu.

Hata mambo yalipokuwa magumu aliibeba timu kama ya kwakwe, hakuwa tu mfanyakazi bali alikuwa sehemu ya wamiliki wa team.

Mambo mengine alifanya kwa uzoefu ila Kuna mengine alifanya kama mama kwa Wachezaji kiasi kwamba naamini Kuna wachezaji wengi hawawezi kumsahau.

Niseme tu ukweli Championship ni ligi ngumu kwa sababu hakuna vyanzo Vya mapato hasa kwa hizi team ambazo haziko chini Ya Majeshi, zinakuwa na mikwamo mingi ambayo wakati mwingine mnahitaji viongozi waelewa na wanaoweza kuongoza vijana mpaka mfikie mafanikio.

Edna Lema Mourinho Kuna wakati aliibeba team na kuna wakati aliamua mambo kama kiongozi mkubwa wa klabu na tulifanikiwa kwa mambo mengi.

Msimu mmoja umekuwa mfupi sana. Wakati tunaenda Play off alinifuata na kuniambia ana offers 3 za team za Premier league na 1 ya Team ya Wanawake tulikubaliana kama Biashara Utd itapanda basi atabaki na team yetu ila kama mambo yataenda tofauti ataangalia offer alizonazo.

Na baada Ya Mechi yetu na Tabora hatukuzungumza ila tulipokutana aliniambia amechagua kurudi Yanga Princess leo imethibitishwa na kweli alikuwa mkweli.

Naamini tutafanya kazi tena pamoja Mdogo wangu. Mungu akusimamie ufanikiwe katika kazi zako. Binafsi nakupenda sana na Natamani kukuona mbali zaidi.

SOMA NA HII  YANGA WAMKUNJULIA ROHO FEI TOTO...JINA LAKE KUTAJWA KWENYE FAINAL YA CAF JUMAPILI...