Home Uncategorized WACHEZAJI WA BARCELONA KUKATWA MSHAHARA

WACHEZAJI WA BARCELONA KUKATWA MSHAHARA


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Klabu ya Barcelona inayoshiriki La Liga nchini Hispania ipo kwenye mpango wa kuwapunguzia asilimia 30 mshahara wachezaji wake wote wanaolipwa pesa ndefu ili kuepuka janga la kufilisika.

Hali hiyo imefikia hapo kutokana na timu hiyo kupitia kwenye kipindi cha mpito hasa kwenye masuala ya malipo kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo limeyumbisha mambo mengi duniani.

Mpaka wiki ijayo habari zinaeleza kuwa mpango huo utakuwa umeanza kutendewa kazi ili kuruhuu utendaji wa masuala mengine kuendelea ndani ya timu hiyo anayocheza staa Lionel Messi na wanahitaji kuokoa Euro milioni 170 watakapofanya hivyo.

Kwa mujibu wa Mundo Deportive, imeripoti kuwa tayari kikwazo cha kwanza ambacho ni kuhusu mshahara wa wachezaji wao wanaolipwa pesa ndefu ili kuweza kuweka usawa katika hali ya uendeshaji wa timu kimepenya na ripoti imeongeza kuwa wachezaji ambao watabaki watafanya nao mazungumzo kuhusu malipo yao

Kwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha sasa wengi wameonekana kukubali ikiwa ni pamoja na nyota wanne ambao ni pamoja na  Marc-Andre ter Stegen, Frenkie De Jong, Clement Lenglet  na Gerard Pique. 

Antoine Griezmann  ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mrefu ambao ni Euro milioni 15.3 kwa mwaka huku  Philippe Coutinho akiwa ni miongoni mwa nyota waliokubali kupunguziwa mshahara wake.  

Rais wa Umoja wa Wachezaji nchini Hispania, (AFE), David Aganzo amesafiri mpaka Barcelona ili kuonana na Rais wa Barcelona ili kujadili kuhusu suala hilo.

Miongoni mwa dili ambalo linawapasua kichwa ni pamoja na malipo ya nyota wao Messi ambaye mpango wake namba moja ulikuwa ni kusepa ndani ya kikosi hicho kwa msimu huu ila dili hilo lilikwama kutokana na gharama za uhamisho wake kuwa kubwa.



SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI LA AZAM FC DHIDI YA TRANSIT CAMP