Home Habari za Yanga Leo MZIZE ATABIRIWA MAKUBWA…EDO KUMWEMBE ATOA NENO

MZIZE ATABIRIWA MAKUBWA…EDO KUMWEMBE ATOA NENO

habari za Yanga- Mzize

MSHAMBULIAJI wa Yanga Clement Mzize ambaye yupo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amekuwa na kiwango kizuri sana tangu kuanza kwa msimu huu, ambapo kila mechi ya mashindano aliyocheza Yanga amefunga bao.

Mchambuzi wa michezo Legend Edo Kumwembe amemzungumzia mchezaji huyo, na kumtabiria mambo makubwa katika safari yake ya soka.

“Kama akiendelea na moto huu huu atakuwa chaguo la kwanza kwa Stars kwa miaka mingi ijayo wakati huu kina Samatta na Simon Msuva wakielekea ukingoni.”

“Kwa Mzize mwenyewe? Amepiga hatua kubwa. Amepiga hatua kubwa katika maisha yake binafsi. Ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi kote nchini.

“Kutoka kuendesha bodaboda mpaka kuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari Afrika. Muda siyo mrefu ataendesha Range Rover yake binafsi. Ni namna ambavyo maisha yanakwenda kasi.” -Edo Kumwembe.

“Kama Mzize akienda nje akacheza katika klabu imara zaidi ya Yanga, basi kutakuwa na manufaa makubwa kwa taifa. Nadhani anaweza kuwa mshambuliaji namba moja wa Taifa Stars kama tukifuzu kwenda Afcon mwakani pale Morocco.”

SOMA NA HII  BEKI HUYU WA SIMBA APANDISHA MIZUKA SUPER LEAGUE