Home Habari za Yanga Leo GAMONDI AELEZA ALIVYOHUSIKA…KUMBAKIZA MZIZE YANGA

GAMONDI AELEZA ALIVYOHUSIKA…KUMBAKIZA MZIZE YANGA

HABARI ZA YANGA-MZIZE

KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kwamba alihusika katika ushawishi wa kumbakisha mshambuliaji Clement Mzize asiondoke klabuni hapo huku akitaja sababu mbili za uamuzi wake huo juu ya kinda huyo.

Gamondi alisema licha ya ofa ambazo Mzize zimeanza kutajwa akitakiwa na klabu kubwa za Afrika, lakini bado mshambuliaji huyo anatakiwa kubaki ndani ya timu hiyo ili aweze kujiongezea thamani kubwa sokoni.

Mzize ambaye alikuwa anahitajika sana na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco, kwa dau kubwa la usajili lakini bado Yanga wakamuwekea ngumu kuondoka.

Yanga inadai kuwa thamani ya Mzize sio ya Shilingi Milioni 600, bali ana thamani ya kuanzia Bilioni moja, hivyo kama kweli Wydad walikuwa wanamtaka walitakiwa kupandisha dau lao la kumnunua mchezaji huyo.

Lakini pia Clement Mzize bado yupo kwenye mipango ya Yanga, kwa msimu huu kwa mujibu ya kauli ya Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe aliyefunguka kuwa Mchezaji huyo hawezi kuondoka kwenye klabu hiyo kwa sasa.

SOMA NA HII  COASTAL UNION YAZIDI KUWEKA MSIMAMO...YAMUITA KAMBINI LAMECK LAWI