Home Habari za Simba Leo LAMECK LAWI AJUTIA KUIKOSA SIMBA

LAMECK LAWI AJUTIA KUIKOSA SIMBA

Habari za Simba-Lameck Lawi

Ilikuwa rahisi kama ambavyo nilikuwa naamini itakuwa hivyo,ule ukute wa Simba pale nyuma kwa sasa chini ya “Insepector” Chamou Karaboue, Abdlurazack Hamza pamoja na Che Malone bila kumsahau Kazi,nafasi ya Lameck Lawi ilikuwa hainekani hata kwa hadubini kali

Kijana ilitakiwa ajiunge na Simba mapema ili apambanie nafasi,kitendo cha kujichelewesha kutokana na sababu mbalimbali kwa sasa hilo silioni tena kutokea,Simba wamemua kupiga hatua moja zaidi mbele kuhusu kikosi chao

Ikiwa bado hakuna majibu ya moja kwa moja kuhusu shauri lao (Simba na Coastal),kitendo cha mchezaji kujumuishwa kwenye kikosi cha U-20 ya Taifa akiorodheshwa kuwa ni mchezaji wa Coastal kuna majibu unayapata kabla ya hata ya kuulizwa swali lolote

Kama Lawi hatocheza vilabu vikubwa vya Kariakoo kwenye “Career” yake,tukio la kuikosa nafasi ya kucheza Simba kama ilivyomtokea itakuwa moja ya stori tamu katika siku za usoni tukikaa na wajukuu zetu kuwasimulia !!.

SOMA NA HII  JOHN BOCCO KUFANYA SAPRIZI KABLA YA SIMBA DAY