Home epl MANCHESTER UNITED YAPINDUA MEZA KIBABE

MANCHESTER UNITED YAPINDUA MEZA KIBABE

 LICHA ya Bertrand Traore wa Aston Villa kupachika bao la kuongoza dakika ya 24 haikuwafanya Manchester United kuondoka kinyonge kwani walipindua meza na kusepa na pointi tatu. 

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Villa Park ulisoma Aston Villa 1-3 Manchester United. 

Ni Bruno Fernandes dakika ya 52 alipachika bao hilo kwa penalti, Mason  Greenwood dakika ya 56 na Edinson Cavani alipachika msumari wa mwisho dakika ya 87.

Olle Watkins dakika ya 89 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Villa kukamilisha dakika 90 wakiwa pungufu.

Ushindi huo unaifanya United kufikisha jumla ya pointi 70 nafasi ya pili huku Aston Villa ikiwa nafasi ya 11 na pointi 48 vinara ni Manchester City wakiwa na pointi 80.


SOMA NA HII  LIVERPOOL WAIBWAGA MAN UNITED KWA NUNEZ...APEWA MIAKA 6 YA KUJIVINJARI ANFIELD....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here