KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemtaja kipa, Castor Muhagama amepunguza idado ya mabao ambayo walitakia kushinda katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Jumatano Septemba 25, Yanga ilipata ushindi wake wa pili katika mchezo wa Ligi Kuu kwa kumfunga Ken Gold FC bao 1-0, ugenini uwanja wa Sokoni, Mbeya.
Amesema wametengeneza nafasi nyingi katika mchezo wao na Ken Gold FC na Muhagama anefanya kazi nzuri na kuokoa mipira ya hatari mingi iliyomfikia.
“Tumetawala mpira, uzoefu wa wachezqji wangu tumefanikiwa kupata alama tatu, wachezaji wamepambana kwa sababu Ken Gold walicheza kwa nguvu ,” amesema Gamondi.
Kocha huyo amesema Muhagama amefanya kazi nzuri kwa kusaidia timu yake kuokoa mipira mingi ambayo ililenga lango lake na kuonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Ameongeza kuwa licha ya kupoteza nafasi nyingi za wazi anawapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo wa Ligi mbele ya Ken Gold FC.
Gamondi amesema mchezo ulikuwa mgumu na walitengeneza nafasi nyingi za wazi lakini umakini wa safu ya ulinzi ya wapinzani wao wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0.
Wananchi wamefikisha pointi 6 baada ya mechi mbili huku Ken Gold wakiendelea kusubiri ushindi wa kwanza wa msimu baada ya mechi tano za msimu.