Home Habari za Simba Leo SIFA ZA MCHEZAJI MPYA WA SIMBA ELLIE MPANZU

SIFA ZA MCHEZAJI MPYA WA SIMBA ELLIE MPANZU

2618
0
Simba SC

Nilishuhudia mechi chache za AS Vita msimu uliopita akiwepo Elie Mpanzu, sio sababu yoyote kwanini asiwe tatizo / hatari kwa wapinzani katika michuano ya ndani hadi nje, anasaidia kuboresha / vitu vingi kwa timu yako ( Simba ) / winga yako

  1.   Mchezaji ambaye amebarikiwa sana ufundi miguuni ( zile touch zake, one touch football na ile combination play , kwa maana anakupa leseni ya kucheza eneo finyu na kushinda mipambano )

  2.   Mchezaji ambaye anacheza huku macho yanaangalia juu ( sio yule mchezaji ambaye anafanya runs zake / kusprint akiwa macho sini muda mwingi ) , kitendo hicho kinamfanya aweze kuziona pasi na kuzipiga, gifted player.

  3.   Kasi nzuri inahitajika kwa Mshambuliaji wa pembeni na kuingia ndani ( yani yupo explosive mithiri ya Vini Jr, Rashy , Saka, Dembele na Diaz ) , kwa maana inampa leseni ya kufika katika actions / mpinzani kwa nyakati sahihi.

  4. He can score goals and create them ( anajua kutengeneza nafasi za mabao, na mmaliziaji mzuri tu, yes he can see a pass, keep the ball )

Baada ya kusema haya niseme Elie Mpanzu atakuwa na nafasi kubwa ya kuwapa balance nzuri sana Lunyasi kwa kutawala eneo la pembeni, yani huyu Winga ni silaha kubwa uwanjani.