Home Habari za michezo HUYU HAPA ALIYEHUSIKA 100% USAJILIWA MPANZU SIMBA….

HUYU HAPA ALIYEHUSIKA 100% USAJILIWA MPANZU SIMBA….

Simba SC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kocha Fadlu Davids amehusika kwa asilimia 100 kwenye usajili wa wachezaji wa timu hiyo akiwemo mshambuliaji mpya Ellie Mpanzu.

Jumatatu Septemba 30, saa 5 usiku Simba imemtambulisha aliyekuwa mchezaji wa klabu ya As Vita ya DR Congo, Mpanzu kwa mkataba wa miaka miwili na leo ameingia kambini na timu hiyo kujiandaa na michezo iliyopo mbele yao.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamethibitishwa na Kocha Fadlu meshiriki katika kila hatua ya usajili uliofanya wa Simba.

“Tuliingia makubalino na Kocha Fadlu mapema tulishindwa kumtambulisha mapema kwa sababu alikuwa na mkataba na timu ya awali lakini kipindi chote alikuwa akishiriki katika usajili hata Mpanzu alikuwa chaguo lake la kwanza,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa Mpanzu alikuwa kwenye mipango yao ya muda mrefu, kutokana na changamoto zilizokuwepo nje ya uwezo wao na wamefanikiwa kupata huduma ya nyota huyo.

“Mpanzu atakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba wanaoingia kambini leo kujiandaa na mechi iliyopo mbele yetu, nyota huyo atakuwa sehemu ya timu hiyo,” amesema Ahmed

SOMA NA HII  BAADA YA KUOTEWA NA SIMBA JUZI....HIZI HAPA MECHI KOKI ZA YANGA SC ZILIZOBAKI...WAKIFELI NDIO BASI TENA...