Home news KUHUSU ISHU YA STRAIKA SIMBA KUTAKA KUSEPA…UONGOZI WAIBUKA NA HILI JIPYA…

KUHUSU ISHU YA STRAIKA SIMBA KUTAKA KUSEPA…UONGOZI WAIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Simba

WAKATI Kamati ya hadhi na haki za wachezaji wakifikiria juu ya ufumbuzi wa migogoro ya mikataba kati ya mchezaji na klabu, uongozi wa klabu ya Simba Queens upo kwenye sintofahamu na mshambuliaji wake, Aisha Mnuka aliyeandika barua ya kuondoka ndani ya timu hiyo.

Simba umemtaka mshambuliji huyo bora wa msimu uliopita kufuata taratibu zote ambazo zimeeleza katika mkataba wake kwa klabu nyingine inayohitaji huduma ya mchezaji huyo.

Mshambuliaji bora wa msimu uliopita ambaye ametoweka ndani ya timu hiyo bila taarifa amepeleka barua kwa uongozi wa klabu hiyo kuomba kuondoka kwa kuwa amepata timu kutoka nje na mbili za Tanzania.

Mratibu wa Simba Queens, Selemani Makanya amesema kuwa wamepokea barua hiyo hali ya kutoka kwa Aisha baada ya kupotea kwa muda akitaka kuondoka kwa sababu amepata timu.

“Wakati analeta barua hiyo tayari jina lake lipo kwenye kamati ya nidhamu, lakini utaratibu unajuliaka wa mchezaji mwenye mkataba wa mwaka mmoja anayepata timu nje au ndani ni kufuata taratibu za usajili kutoka klabu moja kwemba nyingine,” amesema.

Makanya amesema mshambuliaji huyo tangu amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa kupewa stahiki zake zote na ikiwemo kulipwa mshahara wake wa kila mwezi hali ya kuwa yupo nje ya eneo lake la kazi kinyume na makubaliano ya mkataba na Simba.

“Hatuwezi kumruhusu kwa kienyeji kama anavyotaka kwa sababu kuna taratibu za mpira wa miguu zimewekwa na kwenye mikataba tunaosaini, amekuwa mtoro kwenye eneo lake la kazi tangu amesajiliwa hajaitumikia mkataba wake unawezeje kumruhusu mchezaji huyo,” amesema Mratibu.

Ameeleza kwa kuwa nyota huyo jina lake lipo kwenye kamati ya nidhamu ambayo inaongozwa na Seleman Kova itakapokutana na kujadili kesi au malalamiko yaliyopo mezani kwao ikiwemo ishu ya mchezaji bora huyo wa msimu uliopita.

SOMA NA HII  DILI LA NTIBAZONKIZA KUTUA SIMBA...MINZIRO APIGILIA MSTARI...AFUNGUKA JAMBO LLIVYO...