Katika hali ya kushangaza kiungo wa klabu ya Simba SC Yusuph Kagoma amefuta picha zake zote akiwa na klabu yake,pamoja na utambulisho wake Kama mchezaji wa Simba SC katika Mtandao wa Instagram (BIO ).
Ikumbukwe Yusuf kagoma alikuwa akiuguza majeraha ambayo yalimuweka nje ya uwanja katika michezo kadhaa ambayo klabu ya Simba wamecheza.
Pia kiungo huyo hajasafiri na timu ya Simba kuelekea nchini Algeria kwenye mchezo wa pili wa Simba hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine.
Yusuf Kagoma alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa mwezi wa nane, ambapo usajili wake ulizua utata wa kuhusishwa na Yanga.
Katika sakata hilo, ilielezwa kuwa Kagoma alikuwa ameshasaini mkataba wa awali na Yanga , hali iliyoibua utata mkubwa ambapo ilibidi TFF kuingilia kati na kumuidhinisha kuichezea Simba.
Hata hivyo Kagoma katika maisha yake ya Simba hajafanikiwa kupata muda mzuri zaidi wa kucheza kutokana na kuumia mara kwa mara, ambapo hivi karibuni alikaa nnje kwa zaidi ya mwezi mzima akijiuguza.
Pamoja na kufuta picha na taarifa ya utambulisho wake kuwa mchezaji wa Simba, bado ameacha picha yake ya kwenye ‘profile’ ikikuonyesha akiwa na jezi ya mabingwa hao wa zamani wa Tanzania.
Ni mapema bado kusema kuwa kuna sintofahamu kati yake na Simba, kwani mara kadhaa baadhi ya wachezaji mastaa hata Ulaya wamekuwa wakifuta utambulisho wa timu zao kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii lakini husalia kuwa wachezaji wa timu hizo.
Kagoma alisaini mkataba wa miaka 3 na Simba, ambapo ndio kwanza katumikia nusu ya msimu hajamaliza bado, hivyo huenda kufanya kwake hivyo ni katika sehemu ya kuweka ‘presha’ katika baadhi ya matakwa ya kimkataba waliyokubaliana na uongozi wa Simba.