Home Habari za michezo KWA KAULI HII YA FADLU…SIMBA MJIANDAE KULA ‘BIRIANI KUKU’ MWAKA HUU 🙈😁….

KWA KAULI HII YA FADLU…SIMBA MJIANDAE KULA ‘BIRIANI KUKU’ MWAKA HUU 🙈😁….

Habari za Simba- Fadlu Davids

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewaambia wanachama na mashabiki wa Simba watarajie makubwa zaidi mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kumaliza raundi ya kwanza kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 40.

Akizungumza juzi  kocha huyo alisema anakwenda kukiboresha kikosi kwa mara nyingine ili kirejee kikiwa bora zaidi ya kilivyokuwa sasa, hivyo mashabiki watafurahi zaidi.

Huku akiwaomba kuendelea kujitokeza kwa wingi viwanjani kila inapocheza, alisema: “Tumemaliza michezo 15, tumevuna pointi 40, napenda kuwashukuru sana mashabiki wa Simba, kila tunapokwenda, kila tunaposafiri tunao na wengine tunawakuta huko.

“Tunataka kufanya kitu kingine kizuri zaidi mzunguko wa pili, tunaiboresha timu na kuendelea kukinoa kikosi kiwe bora zaidi ya mzunguko wa kwanza, hivyo tunawaomba wanachama na mashabiki wote wa Simba kuwa karibu nasi kwa ajili ya kutupa sapoti.”

Fadlu aliendelea kulia na baadhi ya waamuzi kushindwa kulinda wachezaji wake kwa rafu mbaya wanazochezewa, hasa Kibu Denis, ambaye alisema huwa ni mhanga wa kuchezewa rafu za makusudi na wapinzani, lakini waamuzi wamekuwa hawamtendei haki.

“Katika mchezo huu tumenyimwa penalti mbili, Kibu amekuwa muungwana sana, amekuwa akipigwa mabuti, akipigwa viatu na mabeki mbalimbali katika michezo mingi, halindwi, leo hii imekuwa hivyo hivyo, lakini amekuwa akinyanyuka na kuendelea kucheza mpira, waamuzi wanaangalia tu,” alilalamika kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

“Ulikuwa ni mchezo mzuri, nimefurahia kiwango cha wachezaji wangu, hatuwezi kulalamikia uwanja kwa sababu tunatakiwa kucheza kutokana na mzingira tunayoyakuta, tumeumaliza na sasa tunaangalia michuano ya CAF.

SOMA NA HII  MMISRI APEWA MECHI YA YANGA vs MAMELOD....'DATA' ZOTE HIZI HAPA...