Home Habari za michezo RASMIII….KERO ZA CHAMA ZARUDI UPYAA YANGA….KAZI KUANZIA KWA MAZEMBE…

RASMIII….KERO ZA CHAMA ZARUDI UPYAA YANGA….KAZI KUANZIA KWA MAZEMBE…

HABARI ZA YANGA-CHAMA

TAARIFA ikufikie kwamba, nyota watatu wa Yanga, Djigui Diarra, Max Nzengeli na Clatous Chama wamerejea uwanjani wakiwa tayari kuwavaa TP Mazembe.

Yanga wanatarajia kuwa wenyeji wa mchezo huo kesho katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 alasiri huku nyota hao wakiwa tayari kwa mapambano.

Nyota hao wamekosekana katika baadhi ya michezo kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yakiwakabili lakini sasa mastaa hao wamepona na wako tayari kuotetea nembo ya Yanga.

Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe alithibitisha kwa kusema kuwa, baada ya kukaa nje kwa michezo kadhaa, wachezaji hao watatu wamerejea uwanjani kufanya mazoezi ya ushindani.

Amesema vipimo vya madaktari wa timu hiyo vimejiridhisha kuwa, mastaa hao wapo kamili na tayari wanaendelea na mazoezi wakiwa kwenye mipango ya kocha Sead Ramovic kuelekea mechi hiyo ya kesho.

“Hali ya wachezaji hao ipo vizuri, isipokuwa Yao Koussi ambaye bado hajakuwa fiti. Tunaamini kuwa, watakuwa sehemu ya kikosi kitakachowavaa TP Mazembe mechi yetu ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambayo ni muhimu kushinda,” alisema.

Katika michuano hiyo, Yanga wako kundi A linaloongozwa na Al Hilal ya Sudan wenye alama tisa, MC Alger wenye alama nne nafasi ya pili, TP Mazembe nafasi ya tatu wakiwa na pointi mbili huku Yanga akiwa mwisho na alama moja.

SOMA NA HII  CAF WAINGILIA KATI DILI LA MBRAZILI WA SINGIDA BIG STARS KUTUA YANGA...ISHU NZIMA IKO HIVI...