Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIPOTEANA JANA….YANGA WALIA NA HUJUMA….KAMWE AMATAJA ADUI YAO…

WAKATI SIMBA WAKIPOTEANA JANA….YANGA WALIA NA HUJUMA….KAMWE AMATAJA ADUI YAO…

Habari za Yanga leo

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kwa kusema kwamba wanaushindani mkubwa na maadui wakubwa kitakachowanusuru ni umoja, mshikamano na mapambano ya dhati kutoka kwa wanachama wao.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mashabiki na wanachama wanapaswa kuwa pamoja na viongozi wao katika mapambano ya kutafuta alama tatu katika kila michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania ili kutetea mataji yao.

“Ligi ni ngumu sio kwamba msimu umemalizika, yanavyozungumzwa huko nje ni tofauti na uhalisia ulivyo, tofauti ni alama moja kwenye msimamo na bado zaidi ya mechi 10.

Kimsingi bado pointi 30 zipo nje kupigania, tuna nafasi ya kuuchukuwa ubingwa wetu kwa sababu mwisho wa siku tujivunie kile tulichokipata mwisho na sio kupiga hesabu hapa kati kati, ligi bado sana, hivyo wanayanga tusimame na tuzibe masikio yetu,” amesema.

Kamwe amesema wanayanga wasikaribishe maneno yanayozungumzwa na wapinzani wao kwa sababu muda waliokuwa nao wa kutafuta alama tatu kila mechi na mwisho wa msimu majibu ya ubingwa yatakuwa hadharani.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA KUTAKATA MECHI ZA HIVI KARIBUNI..HAYA HAPA MAMBO 5 YA MORRISON USIYOYAJUA..