Home Habari za michezo COASTAL CHAWAKUTA WALICHOKIMBIA SIMBA KWENYE DABI…..

COASTAL CHAWAKUTA WALICHOKIMBIA SIMBA KWENYE DABI…..

Habari za Yanga leo

YANGA imefuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 3-1 huku Maxi Nzengeli akitupia mabao mawili katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo, walitumia dakika 21 tu za kipindi cha kwanza kujihakikishia ushindi huo kwa mabao ya Maxi aliyefunga katika dakika ya 1 na 14, kisha Clement Mzize kupigilia chuma cha mwisho katika dakika ya 21.

Bao la kwanza katika mchezo huo wa hatua ya 32 Bora, Maxi alifunga baada ya kupokea pasi ya Khalid Aucho, kisha kupiga la pili akitengenezewa na Pacome Zouzoua.

Wakati Yanga inachekelea ushindi huo, ghafla beki wa kushoto na nahodha wa Coastal Union katika mchezo huo, Miraji Abdallah alipiga shuti la mbali kutokea nje ya boksi katika dakika ya 18 na kuwaandikia Wagosi wa Kaya bao pekee.

Yanga iliposhtuka kwamba wapinzani wao wanakuja juu wakalitafuta bao la tatu na kulipata katika dakika ya 21, mfungaji akiwa Mzize akimalizia pasi ya Prince Dube na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko wenyeji wakiongoza kwa mabao 3-1.

YANGA KAMA MAZOEZINI

Yanga haikutumia nguvu nyingi kushinda mechi hiyo, kwani ilitawala mchezo kirahisi huku ikipoteza nafasi nyingi za kufunga ikiwabana vyema Coastal Union.

Muda mwingi wa mchezo huo Yanga ilitawala zaidi ikionekana kama ipo mazoezini hali iliyowafanya Coastal Union kuwa kwenye wakati mgumu.

IKANGALOMBO DAKIKA 45 TU

Winga mpya wa Yanga, Jonathan Ikangalombo, alipewa mechi ya pili baada ya ile ya kwanza katika ligi dhidi ya Pamba Jiji kucheza dakika 21, lakini safari hii akiongezewa muda akicheza kwa dakika 45 za kipindi cha pili, akichukua nafasi ya Mzize huku akiingia sambamba na mshambuliaji Kennedy Musonda aliyechukua nafasi ya Dube wakati kipindi cha pili kikianza.

Ikangalombo mambo mawili makubwa aliyoyafanya kwenye mchezo huo ni shuti lake la dakika ya 61 akitengenezewa na Pacome Zouzoua ambalo hata hivyo lilidakwa kirahisi.

Shambulizi jingine alilifanya katika dakika ya 72 akipokea krosi ya beki wa kulia, Israel Mwenda na kujaribu kufunga kwa kubinuka tiktaka lakini mpira alioupiga uligonga besela na kurudi uwanjani.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa timu ya 16 kufuzu hatua ya 32 bora ya michuano hiyo na sasa inakwenda kukabiliana na Songea United.

Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ni Singida Black Stars, KMC, Mbeya City, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania, Mbeya Kwanza, Mashujaa, Pamba Jiji, Stand United, Giraffe Academy, Simba, Big Man, Tabora Utd, Songea FC, Kagera Sugar na Yanga.

Mechi hizo za 16 Bora ili kusaka timu nane za kwenda robo fainali zinaanza Alhamisi hii kwa mechi tatu kabla ya kuendelea tena kesho ambapo bingwa wa michuano hii hukata tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambalo Simba iko robo fainali ikitarajiwa kuvaana na Al Masri ya Misri mapema Aprili.

RATIBA 16 BORA

Singida BS vs KMC FC

Mbeya City vs Mtibwa Sugar

JKT Tanzania vs Mbeya Kwanza

Mashujaa vs Pamba Jiji FC

Stand Utd vs Giraffe Academy

Simba vs Big Man

Tabora United vs Kagera Sugar

Yanga vs Songea FC

SOMA NA HII  DK KADHAA KABLA YA YANGA KUKIPIGA NA WATUNISIA...MTOTO WA NABI AJITOKEZA NA HILI....BABA YAKE AKIFELI NDIO BASI TENA...