Home Habari za michezo PAMOJA NA KUOMBA MSAADA WA πŸΈπ“†….AL MASRY ‘WACHENYETWA’..SIMBA AKIANDIKA REKODI..

PAMOJA NA KUOMBA MSAADA WA πŸΈπ“†….AL MASRY ‘WACHENYETWA’..SIMBA AKIANDIKA REKODI..

Habari za Simba leo

HISTORIA imeandikwa! Mnyama ameenda nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Al Masry ya Misri kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Na muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa robo fainali, mashabiki wa timu hiyo wakawa wanatamba kwamba wanamtaka mpinzani mwingine ili waende zao fainali.

Simba imefuzu nusu fainali ya michuano ya CAF ikiwa ni baada ya kupita takribani miaka 32, tangu mara ya mwisho icheze fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, michuano ambayo mwaka 2004 iliunganishwa na ile ya Kombe la Washindi na kuzaliwa Kombe la Shirikisho Afrika ambayo ndiyo hii Simba imefuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza.

Awali, Simba ilipoteza mchezo wa robo fainali ya mkondo wa kwanza ikiwa ugenini Misri kwa mabao 2-0, lakini nyumbani ikalipa kichapo hicho ambapo dakika tisini zilimalizika kwa Simba kushinda 2-0, matokeo yaliyofanya jumla kuwa 2-2.

Wakiwa na rekodi nzuri nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Simba waliingia na kauli yao mbiu β€˜Hii Tunavuka’ kufuatia kuwa na wastani wa kufunga mabao mawili kwenye kila mchezo tangu raundi ya kwanza ya michuano hii jambo ambalo limewabeba na kuvunja mwiko.

Katika mikwaju ya penalti, utulivu waliokuwa nao wachezaji wa Simba katika upigaji uliwafanya kufunga zote nne kupitia Jean Charles Ahoua, Steven Mukwala, Kibu Denis na Shomari Kapombe.

Al Masry walipata penalti moja kupitia Fakhreddine Ben Youssef, huku Mohamed Hussein β€˜Mido’ na Mahmoud Awad Hassan Elsayed mikwaju yao ikiokolewa na kipa Moussa Camara.

MECHI ILIVYOKUWA

Ndani ya dakika 45 tu za kipindi cha kwanza, vijana hao wa Fadlu Davids walipindua meza huku wakimiliki mchezo huo kwa zaidi ya asilimia 60, walipiga mashuti 15 kuonyesha walikuwa wakiihitaji nusu fainali, mashuti manne yalilenga lango na moja likawapa uongozi. Al Masry ikipiga mashuti manne na mawili yakilenga lango.

Ilikuwa dakika ya 22 ambapo Elie Mpanzu aliachia mkwaju ambao ulimshinda kipa wa Al Masry, Mahmoud Ahmed β€˜Gad’ baada ya kupokea pasi ya Shomary Kapombe na kuifungia Simba bao la kwanza.

Bao hilo liliongeza morali kwa Simba ambayo iliendelea kutengeneza mashambulizi mfululizo kupitia maeneo yote ya uwanja, pembeni ambako walikuwa wakicheza Mpanzu (kushoto), Kibu Denis (kulia) huku Charles Jean Ahoua akiwa nyuma ya Steven Mukwala.

Dakika 11 baadae, Simba ilipata bao la pili kupitia kwa Mukwala aliyejitwishwa kichwa krosi ya Mohammed Hussein. Matokeo hayo yaliifanya Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

SOMA NA HII  DABI YA WANAWAKE....YANGA PRINCESS 'WAIKUNYUGA' SIMBA QUEENS...WAFUTA UTEJA...