Home Habari za michezo PACOME KUSALIA YANGA…? HII HAPA TAARIFA ZA NDAAANI KABISA KUHUSU HATMA YAKE…

PACOME KUSALIA YANGA…? HII HAPA TAARIFA ZA NDAAANI KABISA KUHUSU HATMA YAKE…

Habari za Yanga-Pacome

OFISA Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, amethibitisha kuwa uongozi wa klabu hiyo uko katika hatua za kuhakikisha wachezaji muhimu waliomaliza mikataba yao wanasalia ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano mbalimbali, yakiwemo ya ndani na ya kimataifa.

Kamwe ametaja baadhi ya nyota ambao wanafanyiwa kazi ili wabakie kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuwa ni pamoja na kiungo mkabaji Khalid Aucho, mshambuliaji hatari Pacome Zouzoua na winga mwenye kasi Max Nzengeli.

Amesema licha ya nyota hao kutakiwa na timu nyingine, uongozi uko makini kuhakikisha hawapotezi wachezaji muhimu waliotoa mchango mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo.

“Naomba niwaeleze ukweli Wanayanga tuna vita kubwa. Kuna watu wanahitaji wachezaji wetu ili kuidhoofisha klabu yetu,” amesema Kamwe kwa msisitizo, akionesha dhamira ya klabu kusimama kidete dhidi ya hujuma kutoka kwa wapinzani wanaowinda nyota wa Yanga.

Katika hatua nyingine, Kamwe amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kushiriki kwa vitendo katika uimarishaji wa klabu kwa kulipa ada ya uanachama ya shilingi 24,000 kwa mwaka.

Ametoa wito huo akisema kuwa endapo watapata wanachama milioni moja wanaolipa ada hiyo, klabu inaweza kukusanya shilingi bilioni 24 ambazo zitasaidia katika kuboresha kikosi na kuleta nyota wapya.

Kamwe amesema kuwa fedha hizo zitakuwa msingi wa kuandaa kikosi imara kitakachoshindana kwa mafanikio katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, huku akisisitiza kuwa sasa ni muda wa Wanayanga kujitokeza kwa wingi na kuchangia maendeleo ya timu yao pendwa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGA 'TUGOLI TUMOJA' CHIRWA NAYE AANZA TAMBO ZA UFUNGAJI BORA ETI...