Home Habari za michezo MASHINE MBILI MPYA SIMBA HIZI HAPA….’MAJAMAA’ YANAPIGA KAZI HATARI…..

MASHINE MBILI MPYA SIMBA HIZI HAPA….’MAJAMAA’ YANAPIGA KAZI HATARI…..

Habari za Simba leo

SIMBA inaendelea kujifua kambini jijini Cairo, Misri chini ya kocha Fadlu Davids, lakini kuna mashine mbili mpya zinasubiriwa huko ili kuungana na wenzao walitangulia mapema.

Awali Simba ilipiga kambi ya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya katika mji wa Ismailia, kisha ikahamia Cairo ilipo kwa sasa ikiwa imeshacheza mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu, lakini kuna mastaa wawili wanadaiwa wameshasaini mkataba kitambo wakiwa Dar es Salaam.

Nyota hao ni kipa Yakoub Suleiman na beki Wilson Nangu waliokuwa katika majukumu ya Taifa Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN) 2024 wakitokea klabu ya JKT Tanzania, inadaiwa kwa sasa wanasubiri simu za mabosi wa timu hiyo, ili kujiunga na Simba.

Ipo hivi. JKT Tanzania ilitoa sharti kwa Simba ili iwaruhusu Nangu na Yakoub kujiunga nao, ilitakiwa itoe pesa na wachezaji watatu kwa mkopo ambao ni David Kameta ‘Duchu’, Awesu Awesu na Valentino Mashaka ambao wapo kambini nchini Misri.

Chanzo cha ndani kimesema kuwa kuhusu Nangu na Yakoub bado hawajaambiwa chochote na uongozi wa JKT Tanzania kama watatakiwa kuondoka kwenda Misri kujiunga na Simba, ukimya huo utawalazimu wachezaji hao kwenda katika kambi ya Arusha.

“Simba ilifanya mazungumzo na JKU ambayo ni mwaajiri wa Yakoub kijeshi, lakini iliambiwa iingize pesa kwa mchezaji, JKU na JKT Tanzania ambayo ilikuwa na kipa huyo aliyemaliza msimu uliyopita na clean sheets 10 sasa jukumu la kumruhusu mchezaji lipo kwa JKT,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kuhusu Nangu mwenye mkataba wa kumalizika mwaka 2028 moja ya sharti ni Simba kuwatoa wachezaji wao kwa mkopo, hivyo bado JKT Tanzania ndiyo inatakiwa iwaruhusu kuondoka.”

Klabu ya Simba imetajwa kumalizana na wachezaji hao na walikuwa wakiwasubiri wamalize majukumu yao na Taifa Stars iliyotolewa robo fainali ya CHAN 2024 ili wapandishwe ndege kuwahi kambi iliyopo jijini Cairo, Misri chini ya kocha Fadlu Davids.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA KMC ..NABI KAKUNA KIDEVU WEEEH..KISHA AKASEMA HAYA..