Home Meridianbet MERIDIANBET NA ODDS ZA KUFA NA KUPONA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA…

MERIDIANBET NA ODDS ZA KUFA NA KUPONA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA…

Meridianbet

Mashabiki wa soka barani Ulaya wanapata burudani ya kiwango cha juu huku michuano ya UEFA World Cup Qualification ikizidi kushika kasi. Timu mbalimbali zimeingia uwanjani kuwania nafasi ya kushiriki kwenye Kombe la Dunia, na usiku wa leo kuna michezo mikali inayotarajiwa kutikisa viwanja tofauti barani humo. Kwa mashabiki wa kubashiri, huu ni wakati mzuri zaidi wa kuchangamkia fursa hizi kupitia Meridianbet.

Katika Kundi C, macho yote yatakuwa kwa Belarus watakapovaana na Denmark saa 3:45 usiku. Wadenish wakiwa na historia ya kufanya vyema kwenye michuano mikubwa, wanatarajiwa kupambana vilivyo kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu. Wakati huohuo, Scotland watajaribu kutumia faida ya uwanja wa nyumbani dhidi ya Ugiriki, mchezo unaotarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili. Odds kabambe zipo kwenye mchezo huu.

Michezo ya Kundi G pia inatoa ladha yake. Finland wataikaribisha Lithuania saa 1:00 jioni katika pambano la mapema, kabla ya Malta kuingia uwanjani kuwakaribisha vijana wa Ronald Koeman, Uholanzi, timu ambayo kila mara huleta upinzani mkubwa kutokana na nguvu ya safu yao ya ushambuliaji.

Meridianbet haiishii hapa, kuna michezo mingine ya kasino mtandaoni na mechi za vilabu za kubashiri zenye odds kabambe zinazokupa nafasi ya kuongeza kipato kila siku. Kujiunga ni rahisi mno, tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10# na uanze safari yako ya ushindi.

Katika Kundi H, Austria wanatarajiwa kuwa na kibarua chepesi dhidi ya San Marino, huku Cyprus wakipambana na Bosnia & Herzegovina kwenye mechi ambayo huenda ikawa na ushindani wa hali ya juu kutokana na ubora wa pande zote mbili.

Usiku utamaliziwa na michezo kutoka Kundi L, ambapo Czechia watamenyana na Croatia katika mchezo wa majirani wa Balkan ambao daima huwa na ladha ya kipekee. Mchezo mwingine wa kundi hilo utawakutanisha Faroe Islands dhidi ya Montenegro, mechi ambayo kila pointi ni muhimu kwa matumaini ya kusalia kwenye mbio za kufuzu.

Vita vya kufuzu Kombe la Dunia vinaendelea, na kila bao lina thamani kubwa. Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia usiku mwingine wa burudani, ushindani, na hisia kali za soka barani Ulaya, huku Meridianbet ikihakikisha kila mchezaji ana nafasi ya kuwa mshindi.

SOMA NA HII  MERIDIANBET:BURUDIKA NA MECHI ZA IJUMAA YA LEO