Home Azam FC HUKO AZAM KUNAWAKA MOTO….IBENGE AKUNA KICHWA KWA MASTAA HAWA….

HUKO AZAM KUNAWAKA MOTO….IBENGE AKUNA KICHWA KWA MASTAA HAWA….

455
0
Habari za Michezo leo

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, ameonesha kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa umaliziaji wa kikosi chake licha ya timu hiyo kulazimishwa sare tasa dhidi ya Singida Black Stars, mchezo ambao Azam walitengeneza nafasi nyingi za wazi.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu jana, Ibenge alisema kikosi chake kilipaswa kuondoka na ushindi mnono kutokana na idadi ya nafasi walizozipata, akisisitiza kuwa walistahili kufunga “zaidi ya mabao matatu” lakini ukosefu wa umakini uliwanyima matokeo.

“Tulitengeneza nafasi nyingi sana za kufunga, zaidi ya tatu ambazo zilipaswa kuwa mabao ya moja kwa moja. Lakini hatukufanikiwa. Hii inaonesha bado tunahitaji kufanya kazi zaidi,” alisema Ibenge.

Alipoulizwa kuhusu chanzo cha dosari hizo ikiwa ni uchovu, mbinu au uwezo binafsi wa wachezaji Ibenge alitaja ukosefu wa umakini na maamuzi mabaya ndani ya eneo la hatari kama tatizo kubwa.

“Tatizo ni ‘concentration’. Wachezaji wanafika kwenye boksi lakini wanachukua maamuzi yasiyo sahihi wakati anapaswa kupiga, anapiga wakati anapaswa kupasia, au anajaribu ‘dribble’ isiyo na ulazima. Tunahitaji kuboresha hilo,” aliongeza.

Kocha huyo amesema wataendelea kufanya kazi ya kuboresha maamuzi ya wachezaji kwenye eneo la mwisho ili kuhakikisha nafasi wanazozitengeneza zinageuka kuwa mabao katika mechi zijazo.