Home Habari za michezo STARS HAITAKUWA KINYONGE AFCON 2025, ALI KAMWE

STARS HAITAKUWA KINYONGE AFCON 2025, ALI KAMWE

37
0

OFISA Habari wa Yanga,  Ali Kamwe amewataka mashabiki wa soka nchini Tanzania kuondoa hofu juu ya ugumu wa kundi la Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2025, akisisitiza kuwa mwaka huu mambo yatakuwa tofauti.

Kwa mujibu wake, Tanzania imepiga hatua kubwa na sasa ina uwezo wa kushindana na timu yoyote itakayokutana nayo katika hatua ya makundi.

Kamwe amesema Taifa Stars ina wachezaji waliokomaa kiakili na kimichezo, hali inayowapa ujasiri wa kuingia AFCON bila presha. Ameeleza kuwa enzi za Tanzania kuonekana kama timu ya kujaza idadi zimepita, kwani sasa msingi wa ushindani umewekwa imara.

“Sababu kubwa ya kuamini kikosi cha sasa ni uzoefu wa wachezaji wake, ambao wengi wao wanashiriki mara kwa mara katika michuano ya CAF ngazi ya klabu.

Ushiriki huo, umewapa wachezaji uwezo wa kucheza mechi zenye presha kubwa na kukutana na wapinzani wenye viwango vya juu barani Afrika,” amesema.

Kwa mujibu wa Kamwe, wachezaji hao wanapokutana kambini huleta uzoefu walioupata kutoka klabu zao, jambo linaloongeza ushindani wa ndani na kuinua kiwango cha timu kwa ujumla. inaifanya benchi la ufundi kuwa na chaguo pana na kuongeza ushindani wa nafasi ndani ya kikosi.

Ameongeza  kuwa maandalizi ya mapema na mechi za kimataifa za kirafiki zitakuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Taifa Stars.  kuwa mechi hizo zitawasaidia wachezaji kuzoeana zaidi, kurekebisha mapungufu na kuingia AFCON wakiwa na umoja na maelewano ya hali ya juu.

Kamwe anaamini AFCON 2025 itakuwa jukwaa la Taifa Stars kuandika historia mpya.  mwaka huu Tanzania haitakuwa kinyonge, bali mpinzani wa kuogopwa, mwenye uwezo wa kupigania alama na kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.