Home Habari za michezo SIMBA KUREJEA KAMBINI MAPINDUZI 2026

SIMBA KUREJEA KAMBINI MAPINDUZI 2026

34
0

KIKOSI  cha Simba kinatarajiwa kurejea kambini kesho Jumapili, Desemba 28, 2025 kuanza rasmi maandalizi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 yatakayofanyika Zanzibar.

Hatua hiyo inaashiria mwanzo wa safari mpya kwa Wekundu wa Msimbazi katika moja ya mashindano muhimu ya maandalizi kabla ya kuendelea na majukumu mengine ya msimu.

Baada ya mapumziko mafupi, wachezaji wote ambao hawapo katika majuku ya timu za Taifa wanatarajiwa kuingia  kambini wakiwa katika hali nzuri ya utayari, huku benchi la ufund linaloongozwa na Steve Berker  likilenga kurejesha uimara wa kikosi kimwili na kiufundi.

Maandalizi hayo yatakuwa muhimu kwa Simba kujipima dhidi ya wapinzani tofauti watakaoshiriki mashindano hayo na kijiandaa na michuano iliyopo mbele yao.

Simba itaanza kampeni yake ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza mechi ya kwanza Januari 3, 2026 dhidi ya Muembe Makumbi.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, ambao kwa miaka mingi umekuwa kivutio kikubwa cha mashindano hayo kutokana na hamasa ya mashabiki.

Mchezo dhidi ya Muembe Makumbi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo imekuwa ikionesha maendeleo na kujiamini katika mashindano ya ndani.

Simba itahitaji umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha inaanza vyema mashindano hayo.

Kwa upande wa wachezaji, kikosi kinatarajiwa kuwa na mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na chipukizi, huku benchi la ufundi likipata nafasi ya kuwapima baadhi ya nyota wapya pamoja na kurejesha ushindani wa nafasi ndani ya timu.

Mashabiki wa Simba wanaendelea kuonesha hamasa kubwa kuelekea mashindano hayo, wakiamini kuwa timu yao itaonesha kiwango kizuri na kupambana kuwania taji hilo. Kombe la Mapinduzi limekuwa jukwaa muhimu kwa Simba kuimarisha mbinu na morali ya kikosi.

Kwa ujumla, kurejea kambini na maandalizi ya Mapinduzi Cup 2026 ni fursa muhimu kwa Simba  kujijenga upya, kusahihisha mapungufu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo ya ndani na kimataifa.