Home Habari za michezo SILAHA MPYA YANGA KUITUIKIA FAINALI YANGA MAPINDUZI

SILAHA MPYA YANGA KUITUIKIA FAINALI YANGA MAPINDUZI

48
0

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa upo tayari kuwatumia wachezaji wake wapya waliosajiliwa hivi karibuni katika michezo ya hatua za juu ya Kombe la Mapinduzi linaloendelea visiwani Zanzibar.

Yanga tayari imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo ya awali, hali inayowaweka katika nafasi nzuri ya kupigania taji hilo.

Katika hatua ya nusu fainali, Yanga inatarajiwa kuivaa Singida Black Stars Januari 9, 2025, kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema mashabiki wa Yanga wanapaswa kutarajia kuona mabadiliko ndani ya kikosi, ikiwemo uwezekano wa kuonekana kwa wachezaji wapya kuanzia nusu fainali hadi fainali.

Kamwe amesema  uwepo wa wachezaji wote kambini, wakiwemo waliosajiliwa hivi karibuni, umeipa benchi la ufundi uhakika mkubwa wa kupanga kikosi chenye ushindani.

“Hii ni hatua muhimu kwetu na tunakwenda kukutana na wapinzani wenye uwezo, lakini wachezaji wote wapo tayari, hata wale wapya, hivyo yeyote tutakayekutana naye atapata wakati mgumu,” amesema  Kamwe.

Yanga inaingia kwenye hatua hizi za maamuzi ikiwa na dhamira ya kutwaa Kombe la Mapinduzi, huku wachezaji wapya wakitajwa kuwa silaha muhimu katika kufanikisha azma hiyo.