Meridianbet Tanzania imeonesha tena dhamira yake ya kugusa maisha ya Watanzania kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kwa kutoa msaada wa fimbo za kutembelea kwa watu wenye ulemavu wa kuona jijini Dar es Salaam. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika ofisi za Tanzania Association of the Blind (T.A.B) zilizopo Kinondoni, na kuhudhuriwa na viongozi na wanachama wa taasisi hiyo pamoja na wawakilishi wa Meridianbet.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Uhusiano wa Umma wa Meridianbet, Nancy Ingram aliyekuwa ameongoza timu ya kampuni hiyo, alieleza kuwa msaada huo unatokana na falsafa ya Meridianbet ya kuamini katika kurudisha kwa jamii kama sehemu ya utamaduni wake wa uendeshaji. Alisisitiza kuwa kampuni inaona wajibu wake si tu katika kutoa huduma bora, bali pia kushiriki kikamilifu katika kuboresha ustawi wa makundi yenye uhitaji maalum.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Mwenyekiti wa T.A.B aliipongeza Meridianbet kwa mchango huo, akibainisha kuwa fimbo hizo ni nyenzo muhimu kwa watu wasioona katika kuhakikisha wanatembea kwa usalama na kujiamini zaidi. Alisema msaada huo utaongeza uhuru wa wanachama wao katika shughuli za kila siku na kuwapa motisha ya kuendelea kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.
Kwa upande wa Meridianbet, tukio hilo limekuwa sehemu ya mfululizo wa miradi ya kijamii inayolenga kusaidia watu wenye ulemavu na makundi mengine yenye changamoto. Kampuni imekuwa ikiwekeza katika mipango inayochochea usawa, ujumuishi na upatikanaji wa fursa sawa kwa wote.
Kupitia msaada huu, Meridianbet imeonesha kwa vitendo kuwa inaamini katika kujenga jamii inayothamini utu na ushirikiano. Kampuni imeahidi kuendelea kushirikiana na taasisi kama T.A.B ili kuleta mabadiliko endelevu na kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata msaada na heshima wanayostahili katika jamii.