Home Habari za michezo YANGA YAJA NA MBINU MPYA, SIMBA PABAYA FAINALI YA MUUNGANO

YANGA YAJA NA MBINU MPYA, SIMBA PABAYA FAINALI YA MUUNGANO

0

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amefichua mbinu wanazopewa na kocha wao, Pedro Goncalves, kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Simba.

Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, ambapo mahasimu wakubwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na Yanga, watakutana kuwania taji hilo.

Mwamnyeto amesema kikosi chao kipo tayari kwa pambano hilo muhimu, akisisitiza kuwa maandalizi yamezingatia kwa kina ubora na udhaifu wa wapinzani wao.

Ameeleza kuwa benchi la ufundi chini ya Goncalves limefanya uchambuzi wa kina wa mchezo wa nusu fainali wa Simba, jambo lililosaidia kubaini maeneo ya kushambulia na kujilinda.

“Kocha amewafuatilia wapinzani wetu kwa dakika 90 katika mchezo wao wa nusu fainali, ameona ubora na madhaifu yao na kuyafanyia kazi mazoezini ili tuwe tayari zaidi,” amesema Mwamnyeto.

Ameongeza kuwa morali ya wachezaji ipo juu, huku wakilenga kupambana kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanatetea ubingwa wao na kuondoka na ushindi katika fainali hiyo.