Habari za michezo

SIMANZI MBWA WA WEMA SEPETU MANUNU AMEKUFA AACHA GUMZO MITANDAONI

Vardo May 4, 2026 8:46 pm

Tasnia ya burudani nchini imegubikwa na simanzi baada ya taarifa za kifo cha mbwa wa msanii wa Bongo, Wema Sepetu, aliyefahamika kwa jina la Manunu.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Wema alithibitisha kuondokewa na mnyama huyo aliyekuwa akiishi naye kwa zaidi ya miaka sita, akionyesha wazi maumivu ya kumpoteza rafiki na “mtoto” wake wa karibu.

“Siyo rahisi kwangu… Manunu alikuwa sehemu ya maisha yangu kila siku,” ameandika Wema.

Manunu alikuwa zaidi ya mbwa wa kawaida. Umaarufu wake ulijengwa kupitia uwepo wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ma Wema alikuwa akishirikisha picha na video zilizoonyesha maisha yake ya kila siku, jambo lililomfanya kupendwa na kufuatiliwa na maelfu ya watu.

Hata hivyo, umaarufu huo uliambatana na mjadala. Wapo waliovutiwa na kiwango cha mapenzi na malezi aliyokuwa akipewa, huku wengine wakikosoa wakisema uangalizi huo ungeelekezwa zaidi kwa watu wenye uhitaji. Licha ya hayo, mashabiki wengi waliendelea kumtetea Wema.

Tukio lililowahi kuzua gumzo
Mwaka 2021, Manunu aliwahi kupotea nyumbani kwa Wema, tukio lililoibua taharuki mitandaoni. Katika juhudi za kumpata, muigizaji huyo alitangaza dau la Sh1 milioni kabla ya kuliongeza hadi Sh2 milioni ndani ya siku hiyo hiyo.

“Namhitaji mbwa wangu arudi… naongeza dau hadi milioni mbili, yeyote atakayemuona anisaidie,” aliandika Wema wakati huo.

Tukio hilo liliongeza zaidi umaarufu wa Manunu na kuonyesha namna alivyokuwa na thamani kubwa kwa mmiliki wake.

Maisha ya kipekee ya Manunu

Mbwa huyo pia alijulikana kwa kuishi maisha yaliyowavutia wengi, ikiwa ni pamoja na: Kupelekwa saluni mara kwa mara kwa ajili ya usafi na urembo
Kuvalishwa mavazi maalum, hasa yenye rangi ya pinki
Kuwa na akaunti yake ya Instagram yenye maelfu ya wafuasi
Kuambatana na Wema katika baadhi ya shughuli zake za kazi
Kuwa na kitanda chake maalum na ratiba ya maisha iliyopangiliwa.

Kwa mujibu wa Wema, Manunu alikuwa kama mtoto wake:
“Watu wanaweza kuona ni mbwa tu, lakini kwangu ni familia,” aliwahi kueleza.

Pigo Kubwa
Kifo cha Manunu kimeacha pengo kubwa kwa Wema Sepetu, huku mashabiki na wadau wa burudani wakimiminika mitandaoni kumpa pole.
Wengi wameeleza kuguswa na uhusiano wa kipekee uliokuwepo kati ya muigizaji huyo na kipenzi chake, wakikiri Manunu alikuwa sehemu ya simulizi ya maisha ya Wema iliyowavutia na kuwaburudisha kwa muda mrefu.

“Pole sana Wema, tunajua ulikuwa unampenda sana,” ameandika shabiki mmoja mtandaoni.

Kwa wengi, Manunu hatabaki kuwa kumbukumbu ya kawaida tu, bali alama ya mapenzi yasiyo na mipaka kati ya binadamu na mnyama wake.

MAMBO 10 USIYOFAHAMU
KUHUSU MBWA WA WEMA SEPETU

Machi mwaka huu mbwa wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu aitwaye Vanilla au Manunu aliteka mazungumzo hasa mtandaoni mara baada ya Wema kutangaza dau la Sh2 Milioni kwa yeyote atayempata mbwa wake ambaye aliyetoweka nyumbani.

Lakini mbwa huyu ni wa aina gani na kwanini amekuwa akipewa kipaumbele kiasi hiki?. Haya ni mambo 10 usiyofahamu kuhusu mbwa huyo wa Wema.

1. Kwa kawaida mbwa Manunu hupelekwa saloni kwa ajili ya usafi na kuboresha muonekano wake walau mara mbili kwa mwezi na anapotolewa saloni huvalishwa vitu miguuni na kwenye mkia ili kumzua asichafuke pindi anapotembea.

2. Rangi anayopenda sana ni Pinki, hii ni kutokana gauni lake la awali kuvalishwa lilikuwa na rangi hiyo, hivyo imemkaa sana kichwani mwake, pia hupenda kuvalia tai Nyekundu.

3. Kuna muda humsindikiza Wema kwenda kushuti filamu, akiwa huko hupenda kusikiliza muziki na kula karanga wakati akimsubiri Bosi wake huyo warudi wote nyumbani.

4. Chakula chake kikubwa ni nyama ambayo tayari imepikwa ingawa anaweza kula mbichi kama mbwa wengine, na hupendelea kunywa Mvinyo baada ya kula.

5. Anapopanda gari na Wema hupendelea kuketi siti ya mbele, na mara kadhaa amekuwa akijaribu kutaka kuendesha ingawa hajawahi kupewa fursa hiyo.

6. Ana ukurasa wake wa Instagram ambapo anafuatiliwa (followers) na watu zaidi ya 23.9k. Watu wengi huonyesha kuvutiwa na mtindo wake maisha.

7. Wema anadai huyu ni sawa na mtoto wake na anampenda sana. “Ndiyo, ananipenda sana, sio kwa sababu ni Mbwa bali kama mtoto wake,” inasema moja ya taarifa kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Manunu.

8. Kuna wakati hupewa fedha kwa ajili ya matumizi yake ya wikiendi tu, na hizo sio chini ya Sh20,000. Hivyo ni yeye kuamua kama ataenda kununua nyama choma au Mvinyo.

9. Ana kitanda chake maalum cha kulalia alichonunuliwa kutoka duka la Pillow Lady na baada ya kula mchana hupenda kulala walau saa mbili kisha kuendelea na mambo yake.

10. Yote uliyosoma ni machache ya yale anayofanyiwa Mbwa huyu, Wema anasema anafanya hivi kwa upendo tu na wale wanamkosoa kwa kusema bora angefanya hivyo kwa watoto wenye uhitaji, wafahamu kuwa sadaka amekuwa akitoa kila wakati ambazo huwenda kufanya hivyo pia.

BARKER ATOA WIKI MOJA KUFUTA UONGOZI WA YANGA ROMMY3D AWATAJA BACCA, DIARRA KAMA NGUZO MUHIMU YANGA