Fadlu ambaye ambaye alianzia njiani na Raja ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 17, akishinda 10 kama ilivyokuwa kwa Pablo, akipoteza mbili na sare sita, vinara hao wakifunga jumla ya mabao 23 na kuruhusu sita.
MOJA KUAMUA
Ubingwa wa msimu huu nchini humo utaamuliwa kwenye mechi ya mwisho iliyosalia kwa kila timu na Raja itakuwa na kibarua nyumbani dhidi ya Wydad Athletic Mei 9,2026, kumbuka dabi hiyo itachezwa bila mashabiki kutokana na vurugu za mashabiki wa timu zote mbili.
Maghreb yenyewe mechi yake ya mwisho itachezwa Mei 10,2026 ugenini dhidi ya Union Touarga ambayo ipo kwenye hatua ya kushuka daraja, ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi ya kwanza.
MTIHANI MWISHO WA LIGI
Fadlu atasubiri hadi mechi hiyo ya mwisho kujua hatma yake na ushindi ndiyo utakaoamua abaki na endapo atapoteza lolote linaweza kutokea kwani Waarabu hawana uvumilivu.
Tusubiri kuona kocha gani wa zamani wa wekundu hao atachukua ubingwa msimu huu nchini humo.