Home Habari za michezo MBIO ZA UBINGWA ZIMECHACHA SIMBA HAWATAKI KUTELEZA TENA

MBIO ZA UBINGWA ZIMECHACHA SIMBA HAWATAKI KUTELEZA TENA

0

BAADA ya siku moja ya mapumziko mafupi, Simba SC imefanya kurejea rasmi katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo muhimu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumapili, Mei 10, 2026.

Simba itakuwa nyumbani katika dimba la KMC Complex uliopo Mwenge kuwakaribisha Tanzania Prisons kusaka alama tatu muhimu kufikia malengo ya kampezi yao ya kushunda michezo tisa zilizosalia ya Ligi hiyo.

Wekundu wa Msimbazi wameanza tena kazi kwa morali ya juu, huku kauli ya “Mnyama amerudi mawindoni” ikitawala mazingira ya mazoezi yao.

Ushindi walioupata katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzanua umeongeza hali ya kujiamini ndani ya kikosi hicho, lakini pia umeongeza presha ya kutopoteza pointi katika kila mechi iliyosalia.

Simba kwa sasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 46, nyuma ya vinara Yanga SC wenye pointi 51, hali inayofanya kila mchezo kuwa kama fainali ya mwisho.

Benchi la ufundi, kinaloongozwa na Kicha Steve Barker linaelewa vyema ugumu wa mchezo wa Jumapili dhidi ya Tanzania Prisons.

Ingawa wapinzani wao wapo kwenye maeneo ya chini ya msimamo, historia inaonyesha timu zinazopambana kuepuka kushuka daraja huwa na nguvu na morali ya ziada mwishoni mwa msimu, jambo linaloweza kuleta ushindani mkali zaidi uwanjani.

Wakati huo huo, ratiba ya ligi inaendelea kuwa na mvuto mkubwa, ambapo Singida Black Stars watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar, huku Coastal Union wakiwa wageni wa Yanga SC katika Uwanja wa KMC.

Mechi hizo zote zinaweza kubadilisha mtiririko wa msimamo wa ligi, jambo linaloongeza presha kwa Simba na Yanga katika mbio za ubingwa.

Kwa sasa, macho na akili zote zipo Msimbazi. Mazoezi yanaendelea kwa kasi, mikakati inaboreshwa, na wachezaji wakiwa na hamasa ya hali ya juu.