Habari za michezo

HANS FLICK AIPA UBINGWA BARCA SAA CHACHE BAADA YA KUFIWA

Vardo May 11, 2026 11:35 am

BARCELONA, HISPANIA: KOCHA  wa Barcelona, Hansi Flick, ameiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa LaLiga kwa kuwachapa mahasimu wao, Real Madrid mabao 2-0, saa chache baada ya kufiwa na baba yake.

Katika mchezo huo wa El Clasico uliopigwa mbele ya maelfu ya mashabiki walioujaza uwanja wa Camp Nou, Flick alionekana akitokwa na machozi kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki na wachezaji walitoa dakika moja ya ukimya kwa heshima ya baba yake aliyefariki usiku wa kuamkia mchezo huo.

Licha ya majonzi aliyokuwa nayo, kocha huyo Mjerumani alikuwa sehemu ya mchezo huo na kuiongoza Barcelona kuibuka na ushindi huo muhimu uliowapa ubingwa wao wa 29 wa LaLiga wakiwa bado na michezo mitatu mkononi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Flick amesema: “Sitaisahau siku hii maishani mwangu. Ulikuwa mchezo mgumu lakini nawapongeza wachezaji wangu kwa moyo wa kupambana. Najivunia sana timu hii.”

Barcelona imekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu kutokana na mfumo wa ushambuliaji wa Flick uliovutia mashabiki wengi na kuifanya timu hiyo kurejea kwenye ubora wake wa zamani.

Mashabiki wa Barcelona walisherehekea kwa furaha ushindi huo huku wakimuonyesha upendo mkubwa kocha wao ambaye alipambana na maumivu ya msiba lakini akaendelea kuipa mafanikio timu hiyo.

SHIKANGWA MISIMU MINNE, MABAO 60 DAKIKA 180 ZA DHAHABU ARSENAL IKIWABEBA WANNE