Habari za michezo

YANGA YAJIKUTA KWENYE WAKATI MGUMU, MOALIN AFICHUA TATIZO

Vardo May 14, 2026 2:18 pm

KOCHA wa Yanga SC, Abdelhamid Moalin amesema licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC, anaamini walikuwa bora zaidi ndani ya uwanja kutokana na namna walivyocheza na kutengeneza nafasi nyingi za mabao.

Moalin amesema changamoto kubwa iliyowakabili kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Airtel, Singida, ilikuwa ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata mbele ya lango, jambo ambalo lilichangia kupoteza mchezo huo muhimu.

Ameeleza kuwa Dodoma Jiji walionyesha umakini mkubwa kwenye umaliziaji kwa kutumia vyema nafasi chache walizopata, tofauti na Yanga ambao walitawala sehemu kubwa ya mchezo lakini wakakosa ufanisi wa kufunga mabao.

“Kimsingi hatukucheza vibaya, tulicheza vizuri zaidi yao lakini hatukutumia nafasi tulizotengeneza. Sitaki kumblaimu mchezaji yeyote,” alisema Moalin baada ya mchezo huo.

Pamoja na kupoteza alama tatu, kocha huyo ameweka wazi kuwa bado ana imani kubwa na kikosi chake, akisisitiza kuwa matokeo hayo hayaondoi uwezo wala malengo ya timu katika mbio za ubingwa msimu huu.

Katika mchezo huo, Dodoma Jiji FC waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Yanga SC, matokeo yaliyozidi kuchochea ushindani wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku vita ya kileleni ikiendelea kuwa ngumu.

ALLARAKHIA APANDISHA TIMU ENGLAND, MNOGA AKIISAKA LEAGUE ONE SIMBA YAJIBU KIJEMBE CHA YANGA KUHUSU UWANJA